The House of Favourite Newspapers

Hawa Ndio Wataamua Mechi Ya Simba na Yanga

Meddie Kagere

LEO saa 11 Jioni p al e kwa Mchina, Uwanja wa Taifa k i l a shabiki na mdau wa soka ninaamini atakuwa amejikamatia siti yake tayari kwa kuangalia mechi ya watani wa Jadi, Simba na Yanga.

 

Mchezo huu unaweza kuuita ‘mathematical match’ yaani mechi ya kimahesabu zaidi ya Simba na Yanga inatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na namna zilivyoanzishwa hadi kufi kia hapa.

 

Mechi hii ni muendelezo wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19, na mara zote hujaza idadi kubwa ya mashabiki kutoka ndani na nje ya Dar es Salaam baada ya kucheza michezo 23, Simba wenyewe wapo nafasi ya tatu na pointi zao 36 walizopata baada ya kucheza michezo 15, ukipiga hesabu utaona wamepitwa pointi 22 na Yanga lakini nao Simba wamecheza mechi pungufu. Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kuibua na kuvuta hisia tofauti kwa mashabiki katika mchezo wa leo;

 

VITA YA KAGERE, MAKAMBO

Macho ya mashabiki wengi yatak uwa kwa washamb u l i a j i wanne, ambao ni Meddie Kagere, Emmanuel
na pengine hata nje ya mipaka ya Tanzania. Kila shabiki anaiangalia timu yake kwa jicho zuri ili mradi kujihakikishia ushindi moyoni, hata makocha wote huwa wana uhakika na ushindi katika mchezo kila zinapokutana timu hizi mahasimu.

Mechi ya mwisho baina ya miamba hii ilipigwa Septemba 30, mwaka jana ambapo Simba ambao ndiyo walikuwa wenyeji watoka suluhu huku kipa wa Yanga, Beno Kakolanya akiwa staa wa mchezo kutokana na kuokoa mashuti mengi sana.

 

Ukiangalia vyema msimamo wa ligi kuu utaona Yanga wapo kileleni wakiwa na alama 58
Okwi wa Simba na wale wa Yanga ni Heritier Makambo na Amissi Tambwe. Siyo siri, hawa ndiyo gumzo na kweli kuna uwezekano mkubwa mmoja wao lazima afunge.

 

Makambo raia wa DR Congo ndiye kinara wa ufungaji katika msimamo wa sasa wa ligi akiwa na mabao 11 akifuatiwa na Myarwanda Kagere mwenye nane kisha Okwi mwenye saba wakati Tambwe yeye anayo sita licha ya mara nyingi kutokea benchi.

 

Makambo hakucheza mechi iliyopita ya ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano wakati Tambwe alicheza na hakufanikiwa kufunga bao lolote.

Kagere mechi yake ya mwisho kufunga ilikuwa ni dhidi ya Mwadui FC ambapo alitupia bao moja na Okwi ambaye alitokea benchi kwenye mchezo huo hakufanikiwa kufunga.

MAKOCHA NAO HOFU TUPU

Kocha wa Simba, Patrick Aussems si ajabu kumuona akaanza na mfumo wa 4-3-3 kwani amekuwa akiupenda sana. Mfumo huo unatoa nafasi kwa Bocco, Kagere na Okwi kutumika kwa wakati mmoja kwenye eneo la ushambuliaji la Simba.

 

Mambo yanapomzidia huwa anabadilika fasta na kwenda na kucheza kwa 4-4-2 anamtoa Kagere halafu Bocco na Okwi wanabaki kama washambuliaji kisha amamuingiza kiungo wa pembeni.

 

Kwa upande wa Yanga, Mwinyi Zahera naye huwa anaanza kwa 4-4-2 kwa maana huanza na mabeki wanne na washambuliaji wawili na akibadilika sana hutumia mfumo wa 4-3-2-1 ambao humuacha Makambo kama mshambuliaji tegemezi. Haitashangaza zaidi kama atatumia mifumo ya 4-3-3 au ule wa 4-1-4-1.

TAKWIMU ZAO

Yanga mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote ikiwa uwanja wa nyumbani, katika michezo 12 wameshinda 11 na kutoa sare mmoja tu, wamefunga mabao 27 na kuruhusu tisa tu hivyo wamejikusanyia pointi 34. Kwa upande wa Simba, wakiwa ugenini msimu huu wamecheza mechi tano, wameshinda tatu, sare mbili mechi 23 ambazo Yanga wamecheza wamefanikiwa kufunga mabao 40 na kufungwa 15 wakati Simba wenyewe katika mechi 15 wamefunga 31 na kufungwa matano tu.

 

Kwenye safu ya ushambuliaji Yanga itawategemea zaidi Makambo na Tambwe au Mrisho Ngassa huku wakisubiri pasi mpenyezo kutoka kwa Feisal Salum na Ibrahim Ajibu.

 

Simba wao macho yao kwa John Bocco na Kagere na wakati wowote Okwi anaweza kufanya mambo na zaidi watategemea pasi za Claytous Chama na wengineo. Ukuta wa Yanga kwa hakika utakuwa chini ya Kelvin Yondani, Andrew Vincent ‘Dante’, Paul Godfrey, Gadiel Michael na golini anaweza kukaa Ramadhan Kabwili. Simba ukuta wake utachagizwa na Pascal Wawa, Juuko Murshid, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Nicholas Gyan na golini kama kawa Aishi Manula ana asilimia kubwa za kuanza.

 

HESHIMA ZAIDI, KISASI KWA MBALI

Mara inapochezwa mechi kama hii, presha zaidi huwa kwa Yanga kwani hata kama ikiwa inafanya vizuri kwenye ligi huwa haiwezi kufurukuta mbele ya Simba. Katika mechi ya mwisho ya ligi msimu uliopita, Yanga ilifungwa bao 1-0 lililofungwa na Nyoni. Kwenye mchezo wa kwanza msimu huu timu hizo zilitoka suluhu. Safari hii Simba inang’ang’ania kuendeleza heshima na kuionyesha Yanga kwamba huko nyuma haikuwa ikibahatisha kuifunga, huku Wanajangwani nao wakitaka kufuta ‘uteja’ wao kwa Simba.

Comments are closed.