HAZARD, JAMES RODRIQUEZ WAWEKWA SOKONI

Eden Hazard

MASTAA Eden Hazard wa Chelsea na kiungo wa Real Madrid, James Rodriguez inasemekana wapo sokoni kuuzwa
na klabu zao kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

 

Hazard, ambaye amegoma kusaini mkataba wa kuendelea kuchezea Chelsea, amekuwa muda mrefu akihusishwa kujiunga na Real Madrid.

 

Naye Rodriguez kwa sasa anachezea kwa mkopo Bayern Munich na klabu hiyo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kumbakiza ghafla.

Hata hivyo, upepo umegeuka kwani Chelsea imemuweka Hazard sokoni na kutaja dau wanalohitaji kwa ajili ya kumuuza wakati Real Madrid inasemekana ipo tayari kupokea ofa za Rodriguez. Chelsea inasemekana ipo tayari kumuuza Hazard kwa kiasi cha pauni milioni 100.

Rodriguez, ambaye amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi Bayern Munich na wakati mwingine kusumbuliwa na tatizo la majeraha naye inasemekana anataka kuondoka Bayern Munich.

 

Arsenal ndio klabu imejitokeza kumtaka Rodriguez na wachambuzi wa mambo ya soka wanadai anaweza kupatikana kwa ada ya pauni milioni tatu. Hata hivyo, Arsenal itapata upinzani mkali kutoka kwa Bayern ambayo imekuwa naye kwa miezi 18 baada ya kumchukua kwa mkopo kutoka Real Madrid.


Loading...

Toa comment