The House of Favourite Newspapers

Heche: Mipaka ya Hifadhi Isifike Maeneo ya Makazi – Video

Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA), John Heche,  ameilalamikia Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya Hifhadhi za Taifa (TANAPA) kuhusu kuweka mipaka ya hifadhi katika maeneo ya mapori tengefu na mbunga za wanyama jambo ambalo amedai kwa sasa wanaweka hadi kwenye shule, zahanati na nyumba za watu wilayani Tarime mkoani Mara.

 

Heche amebainisha hayo wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii huku akiangushia lawama kubwa mamlaka hiyo kwa kuwatoza faini hadi Sh. milioni 100 wafugaji ambao wamekamatwa wakiingiza mifugo yao kwenye maeneo ya hifadhi.

 

Mbunge huyo amedai kuwa kitendo hicho ni unyama kwani mfugaji hawezi kupata Sh. milioni 20 wala milioni 100 kwa ajili ya faini hizo.

MSIKIE HECHE AKIFUNGUKA

Comments are closed.