The House of Favourite Newspapers

Helikopta ya Leicester City Yaanguka na Kuwaka Moto Ikitoka Uwanjani

Image result for Leicester City helicopter crash

HELIKOPTA ya bilionea, mmiliki wa klabu ya soka ya Leicester City ya Uingereza, Vichai Srivaddhnaprabha, imeanguka na kuwaka moto ikiwa inaondoka katika uwanja wa klabu hiyo baada ya kutoka sare ya 1-1 na klabu ya West Ham.

Imeripotiwa kwamba Vichai — baba wa watoto wanne na mwasisi wa kampuni la  King Power International – alikuwa ndani yake.  Mashahidi wamesema waliiona helikopta hiyo ikiyumba baada ya kutoka  eneo la paa la uwanja huo na kisha kuanguka chini.

Image result for Leicester City helicopter crash

 

Comments are closed.