The House of Favourite Newspapers

Herieth: Majirani Wanamtenga Kisa Msanii!

       

NA IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI | MPAKA HOME

WIKI hii safu yako uipendayo ya Mpaka Home iliruka hadi maeneo ya Yombo- Buza, jijini Dar na kukanyaga ndani ya nyumba ya mwanamama mkongwe kwenye uigizaji Bongo, Herieth Chumila.

Mwanamama huyu ambaye mastaa wengi wanapenda kumtumia kama mama kwenye fi lamu mbalimbali, anaishi nyumbani kwake na mumewe aitwaye Sungura Sadalla pamoja na mtoto wake wa kiume na mtoto wa dada yake huku watoto wake wengine wakiwa wameshaanza kujitegemea.

Ni mambo mengi safu hii imezungumza na staa huyu, nisikuchoshe kwa maneno,  twende sambamba:

MAJIRANI WANAMCHUKULIAJE?

“Kusema kweli majirani wamekuwa wakinibagua sana hata kunishirikisha katika vitu vya muhimu kama misiba au hata harusi na yote hiyo wananichukulia labda siwezi kushiriki vitu hivyo kumbe siyo sahihi maana mimi napenda kujumuika na wenzangu na wala siyo naishi kistaa.

MUMEWE AMEIPOKEAJE KAZI YAKE?

“Katika vitu ambavyo najivunia navyo ni kuwa na huyu mume muelewa kwa sababu ananijali na kuithamini sana kazi yangu na yeye amekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu tangu nimejiunga na sanaa.

AMEOKOKA, MUIGIZAJI NA PIA NI MAMA, ANAJIGAWAJE?

“Kwangu hakiharibiki kitu kwa sababu  kila kitu kina muda wake. Naweza kujigawa vyema na kazi zangu za nyumbani na za kisanii na nikapata muda mzuri wa kujumuika mambo ya kanisani kwa ajili ya kumuabudu Mungu.

AMEPANGA AU AMEJENGA?

“Namshukuru Mungu hapa tumejenga hivyo Mungu ni mwema na amekuwa akinipigania mimi na familia yangu kila wakati maana kwa sanaa ya sasa ilivyogeuka, huwezi kusema utaweza kujenga nyumba.

ANAPENDA KUFANYA NINI AKIWA NYUMBANI?

“Napenda sana kuwa bize na usafi  wa nyumbani kwangu na kingine kikubwa napenda kupika hivyo ninapokuwa nyumbani nahakikisha napika chakula mwenyewe.

WOKOVU NA USANII ANAVICHANGANYAJE?

“Kuokoka ni jambo ambalo mtu anaamua kutoka ndani ya moyo wake lakini mimi kuna shida nilipata hivyo nikapata huduma kutoka kwa Nabii Yaspi, nikapona hivyo basi nikaamua kumrudia Mungu japokuwa bado niko kwenye sanaa, kikubwa ni kuangalia matendo yangu.

FILAMU ZINALIPA?

“Hapana kwa kweli, fi lamu zetu unafahamu malipo yake kikubwa hapa mume wangu ndiye kila kitu na yeye kama baba ndiye msimamizi wa kila kitu hapa nyumbani.”

Comments are closed.