Heshima ni uwezo wako wa faragha-2

Karibu mpenzi msomaji wa safu hii pendwa ya XXLove tuendelee kupeana ‘maujuzi’ kwenye nyanja nzima ya uhusiano kwa jumla.

Wiki iliyopita tulianza mada yetu hii ambayo leo nawaletea maoni mbalimbali ya wasomaji walivyopokea mada yetu ya namna ya kuweka heshima kwa mwenzio ambayo hutokana na uwezo wako wa faragha unapokuwa na mwenza wako.

Kwanza nashukuru kwa wale wote waliopiga simu na kutuma ujumbe mfupi kwa kupongeza, ushauri na namna yoyote ya kuboresha safu yetu hii.

Ifuatayo ni sehemu ya ujumbe wa baadhi ya wasomaji ambao walitoa ushauri kuhusu mada hiyo.

ALFAYO NYACHERY WA CHATO GEITA
Kaka nikupe pole kwanza kwa kazi ya kuelimisha jamii, nakuomba uendelee hivyohivyo bila woga maana wengi hawajui hilo.

JINA KAPUNI
Safi sana kwa mada ya heshima yako ni uwezo wako wa faragha, kiukweli mada umeietendea haki sana, Mungu akuongezee maarifa zaidi.

OMAR WA DAR
Asante kaka kwa mada yako nzuri ya wiki iliyopita, nimekuwa mfuatiliaji mkubwa sana, kiukweli wapo watu wanaojua mapenzi ni fedha au ustaa, jambo ambalo halina ukweli wowote.

Unaweza kuwa na fedha lakini kitandani huna kitu, basi fedha hizohizo unazompa mpenzi wako anapelekewa mtu mwingine mwenye uwezo wa kufanya vizuri awapo faragha, wewe ukawa unadharaulika.

JINA KAPUNI- MWANZA
Pole na majukumu ya kazi, mimi ni msichana wa miaka 23, mada ya uwezo wa faragha nimeipenda na mimi niko kati yao. Mpenzi wangu amekuwa akinilalamikia kuwa sijui mapenzi, nimejitahidi sana ila bado hali ni ileile. Naomba unisaidie nifanye nini? Sipendi kuachwa tafadhali.

JINA KAPUNI
Mimi ni msichana mzuri ila sijui nifanye nini ili nimfurahishe mpenzi wangu, kwa maana si lolote wala si chochote ninapokuwa faragha, nahitaji msaada.

JINA KAPUNI
Hongera sana kwa mada zako nzuri, mada ya wiki iliyopita ilinigusa sana kwa kuzungumzia heshima na uwezo wa faragha, Mungu akuzidishie hekima.

Ni matumaini yangu upo vyema, namuomba mwenyezi Mungu akupe afya njema na hekima zaidi. Mada ya wiki iliyopita ni nzuri sana ila sasa hebu tupatie na njia ya kumfurahisha mpenzi wako.

Jina kapuni
Nina mchumba wangu tunaishi wote kwa muda wa miaka 2 sasa, ila bado hajajitambulisha wala hatujafunga ndoa, mwenzangu anataka nimzalie mtoto, mimi sitaki kuzaa nje ya ndoa, ushauri wako ni upi kwa hili?

Mpenzi msomaji wa XXlove ungependa wiki ijayo tujadili kuhusu mada ipi ya uhusiano? Tafadhali tuma maoni na ushauri wako, nasi tutaufanyia kazi.
Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook kujifunze mengi kuhusu mapenzi.


Loading...

Toa comment