The House of Favourite Newspapers

Hezbollah yathibitisha kifo cha kiongozi wake Nasrallah

0

Kundi la Hezbollah nchini Lebanon limethibitisha kifo cha Sayyed Hassan Nasrallah aliyeuliwa kutokana na shambulio la bomu lililofanywa na jeshi la Israel.

Katika taarifa yake kundi hilo limesema litaendelea na vita dhidi ya Israel katika “kuiunga mkono Gaza na Palestina, na kuilinda Lebanon na wakazi wake.”

Israel ilitangaza mapema Jumamosi kwamba imemuua Nasrallah kutokana na shambulio la anga katika kitongoji cha kusini cha Beirut siku ya Ijumaa.

Taarifa hiyo imesema kwamba kiongozi huyo aliuliwa pamoja na kamanda wa kikosi cha kusini cha kundi hilo Ali Karki, pamoja na makamanda wengine.

Kituo cha televisheni cha Hezbollah, Al-Manar kilianza kutangaza aya za Quran baada ya kutangaza kifo cha Nasrallah.

Wizara ya Afya ya Lebanon imesema kwamba karibu watu sita waliuliwa na 91 kujeruhiwa kutokana na shambulio hilo la Ijumaa.

Televisheni ya Lebanon imekuwa ikonyesha uharibifu uliotokana na shambulio hilo huku moshi ukiwa umetanda angani kutoka kwenye majengo yaliyobomolewa kabisa na uchafu uliozagaa mitaani.

Vyanzo vya habari vya Israel vinasema Marekani iliarifiwa muda mfupi kabla ya shambulio la anga la Ijumaa lakini, Waziri wa Ulinzi Llyod Austin anasema Marekani haikupewa onyo la mapema na wala haikuhusika na mashambulio ya Israel huko Beirut.

AMWAGA MACHOZI AKISIMULIA ANAVYOISHI NA WANAYE 6 KWENYE KIBANDA KAMA CHA KUKU JIJINI DAR

Leave A Reply