The House of Favourite Newspapers

DKT. BASHIRU AKIWA CHINA AANIKA KAZI KUBWA ALIYOIFANYA JPM

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,  CCM Dkt. Bashiru Ally amesema serikali ya awamu ya TANO inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa wamejidhatiti kuondoa rushwa nchini na kwa kiasi kikubwa wameanza kuona mafanikio.

 

Dkt. Bashiru amesema hayo katika kaunti ya Shaxian jimbo la Fujian nchini China alipokutana yeye pamoja na ujumbe wake na kufanya nazungumzo na gavana wa kaunti hiyo ya namna gani walivyofanikiwa kuondoa umaskini kwa wananchi wao kwa kiasi kikubwa na uboreshaji wa makazi na miundombinu.

 

Aidha Katibu mkuu Dkt. Bashiru amesema licha ya vita ya rushwa kuwa kubwa na ngumu lakini hawatachoka kwani kupitia ziara ya makada wa CCM nchini China wamegundua uzalendo, nidhamu na uwajibikaji ndiyo uliowafikisha China mbali kimaendeleo.

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Kheri James amesema kupitia ziara hiyo ya mafunzo waliyiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru atahakikisha vijana nchini wanawekewa mazingira rafiki ya kuhakikisha wanatumia vipaji vyao kubuni miradi ya kimaendeleo ili kulisaidia Taifa.

 

Katibu Mkuu wa CCM yupo nchini China na ujumbe wa makada wa chama cha Mapinduzi takribani 20 kwa mwaliko wa chama cha kikomunisti cha China, CPC ili kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi.
Grace Kingalame, Fujian China.

Comments are closed.