Hidaya wa Pepe Kale Afariki Dunia

MWANAMAMA aliyewahi kumtingisha nguli wa muziki nchini Congo Pepe Kale, miaka ya 1990 hadi akamtungia wimbo baada ya kurudi kwao Congo, mwanamama Hidaya Khamisi Mtumwa maarufu Hidaya wa Pepe Kale mkazi wa Arusha amefariki alfajiri ya leo Julai 20, 2021, ambapo mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho nyumbani kwake Kaloleni Arusha.

 

Machi 30, mwaka 2018, mwanaye Leyla Mtumwa aliawa na mumewe aliyefahamika kwa jina la Kema Kasambula katika nyumba wanayoishi Watanzania hao iliyopo eneo la Haringey, Kirkstall Avenue, N17 jijini London nchini Uingereza kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake tukio ambalo lilivuta hisia za Watanzania walio wengi huku mumewe huyo akifungwa jela huko huko Uingereza.

 

 


Toa comment