High School and College Box Concert…GLOBAL KUKIWASHA LEO ALPHA

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo.

LEO Jumamosi, Kampuni ya Global Publishers, inatarajiwa kufanya tamasha la aina yake katika Shule ya Sekondari ya Alpha iliyopo jijini Dar es Salaam.

 

Tamasha hilo limepewa jina la High School and College Box Concert ambalo litakuwa likifanyika katika shule za sekondari na vyuo mbalimbali hapa nchini.

 

Pacific Ibrahim ambaye ni mmoja wa waandaaji wa tamasha hilo, amezungumzia namna ambavyo litakavyokuwa.

DHUMUNI LA TAMASHA

“Kwanza watu wanapaswa kufahamu kwamba hili tamasha linafanyika kwa mara ya kwanza huku dhumuni kubwa likiwa ni kuwapa elimu wanafunzi ambao wanajiandaa kumaliza elimu ya sekondari na kwenda vyuo mbalimbali.

“Mbali na hilo, pia kutangaza bidhaa zinazozalishwa na Global Publishers.

BIDHAA ZENYEWE

“Bidhaa ambazo tunazizungumzia hapa ni magazeti yetu ya Championi,

Spoti Xtra, Ijumaa, Uwazi, Risasi, Amani na Betika. Pia Global TV Online, +255 Global Radio na Global App.

“Tumeona kuja na hiki kitu ili kuzifanya bidhaa zetu kufika mbali zaidi na tumelenga katika shule mbalimbali na vyuoni kwa sababu huko kuna vijana wengi wamekuwa wafuatiliaji wakubwa wa mitandao ya kijamii.

 

WANAFUNZI KUSHINDANISHWA

“Siku hiyo kuna mambo mengi yatafanyika ikiwemo michezo mbalimbali ambayo hii itahusisha wanafunzi wenyewe watakaoshindana, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

“Kwa watakaofanya vizuri katika mashindano hayo, tutawapa zawadi ili kuonyesha kuwa tunathamini vipaji vyao.

 

WATU MAARUFU WATAKUWEPO

“Wanafunzi watapata fursa ya kupata nasaha kutoka kwa wazungumzaji mashuhuri hapa nchini wakiongozwa na Eric Shigongo ambao watazungumza na wanafunzi katika masuala mbalimbali ikiwemo kutatua changamoto zao za kimaisha.

 

GLOBAL APP KUZINDULIWA

“Kwa siku hiyo ya Jumamosi, ndiyo tutaitumia vizuri sana

kwa ajili ya kuizindua Global App ambayo kuna sehemu itakuwa maalum inayowahusu wanafunzi. Humo ndani tutaweka matukio na mambo mbalimbali yanayowahusu wao peke yao. Itaitwa College Box.”


Loading...

Toa comment