HII KALI! WATAPIKA MSIBANI WAKIDAI KUNYWA MAJI YA SUMU

Related image

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima

ZAIDI ya waombelezaji 10 katika msiba wa marehemu Mugusuhi Mwita wa Kitongoji cha Kwinyunyi katika Kijiji cha Matongo Wilaya ya Tarime mkoani hapa, walitapika baada ya kudai kunywa maji yaliyohofiwa kuwa na sumu, Uwazi lilidokezwa.

 

Waombolezaji hao walidaiwa hivi karibuni kunywa maji hayo katika msiba huo huku lawama wakizipeleka kwenye mgodi mmojawapo (jina linahifadhiwa), unaodaiwa kutiririsha maji yenye sumu kwenye makazi ya watu.

 

Samwel Mugusuhi Mwita ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kwinyunyi katika Kijiji cha Matongo, Nyamongo aliliambia Uwazi kuwa yeye ni miongoni mwa waombolezaji waliopatwa na adha hiyo. “Mimi na waombelezaji wa msiba wa marehemu baba yangu, tulitumia maji hapa nyumbani msibani, siku ya Novemba 13, mwaka huu, zaidi ya watu 10 tulianza kutapika, kwa maana hiyo tunahisi maji tuliyokunywa siyo salama,” alisema mwenyekiti huyo.

 

Uwazi liliwasiliana na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Dk Hamid Adinan juu ya tukio hilo na kutaka kujua hatua zilizochukuliwa ambapo alisema: “Ni kweli nimempigia simu mwenyekiti wa kitongoji hicho, Bwana Samwel baada ya kupatiwa namba yake akinielezea hayo.

 

“Nilichokifanya nilichukua hatua za haraka na timu yangu wafike katika msiba huo na kupata maelezo ya wale wote waliopatwa na hali hiyo kisha kuendesha uchunguzi wa kitabibu ili kubaini chanzo chake na baada ya hapo ndipo nitatoa taarifa sahihi,” alisema Dk Adinan.

 

Wakazi wa Vitongoji vya Kegonga ‘B’, Masangora, Kwinyunyi na Nyamirama wa Kijiji cha Matongo walikusudiwa kuhamishwa na mgodi huo baada ya kuwa karibu na eneo hilo ili kuepukana na madhara yanayoweza kuwapata, jambo ambalo halijatekelezwa. Kuachwa huko kumesababisha waendelee kuishi eneo hilo huku malalamiko yao mengi yakiwa ni kuwepo kwa sumu inayotoka mgodini inayowaathiri wao na mifugo.

 

Mgodi huo umewahi kumjulisha Mtendaji wa Kijiji cha Matongo kuwa wangeweka alama za leseni yao ya SML 18/96 kwa ajili ya uchukuzi wa eneo hilo la wakazi wa Vitongoji vya Kwinyunyi, Kegonga ‘B’, Masangora, na Nyamirama lenye ukubwa wa kilometa zake 1.676 la hekta 47 iliyotaarifu umma kuwa wangeendesha upimaji huo Januari 19, mwaka 2015.

 

Mgodi huo uliomba kufanya hivyo baada ya kutanguliwa na maombi ya Oktoba 2, mwaka 2014 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tarime. Hivi karibuni Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa mkoani hapa alitoa tamko kuwa maji yanayotiririka kutoka katika mgodi huo yapimwe na ikibainika yana sumu, basi walioathirika walipwe fidia.

STORI: IGENGA MTATIRO, MARA

Loading...

Toa comment