The House of Favourite Newspapers

Hii Ndio Kauli ya Barbara Simba

0

OFISA Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba SC, Barbara Gonzalez amesema kuwa wamejifunza kuwaheshimu wapenzani wao kwani hakuna dhamana katika mpira wa miguu.

 

Barbara ametoa kauli hiyo baada ya klabu ya Simba SC kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Jwaneng Galaxy ya Botswana na kuondelewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa Aggregate ya mabao 3-3.

 

“Tumejifunza somo la maana. Kamwe usiwadharau wapinzani wako hadi filimbi ya mwisho itakapopulizwa. Bado ninaamini tuna timu nzuri, kuteleza si kuanguka, tutarudi tukiwa na nguvu zaidi” amesema Barbara.

 

Simba iliingia uwanjani katika mchezo huo ikiwa mbele kwa mabao 2-0 walioshinda wakiwa ugenini nchini Botswana na hivyo kufanya kujiamini zaidi.

 

Mpaka dakika 45′ za kwanza zinakamilika Simba walikuwa mbele kwa ushindi wa bao 1-0 (Agg 3-0) lakini mambo yalibadilika dakika chache tu mara baada ya kipindi cha pili kuanza.

 

Jwaneng Galaxy walianza kwa kasi na mashambulizi ya nguvu katika lango la na kuandika bao la kwanza dakika ya 46′ kupitia kwa Rudath Wendell na dakika 60′ Wendell akaweka bao la pili huku Gape Mohutsiwe akimaliza mchezo huo kwa kuweka bao la tatu dakika ya 86′ hivyo Simba kuondelewa katika michuano hivyo kwa sheria ya bao la ugenini.

Leave A Reply