The House of Favourite Newspapers

Hii Ndiyo Nyumba ya Gharama Kuliko Zote Marekani

0

MWENYEWE umepata pesa zako, umeamua kununua kiwanja na kushusha bonge moja la mjengo, labda liwe la milioni mia tatu, unaona kwamba umekamilisha kila kitu, moyo wako umeridhika na unahisi kwamba hakuna kitu kitakachoweza kukurudisha nyuma.

Bilionea Ira Rennert

My bro! Kama umeona milioni mia tatu ni nyingi kujenga nyumba, basi habari ikufikie kwamba nchini Marekani kuna nyumba imetengenezwa kwa gharama ya dola milioni 200 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 450. Si nyumba ya serikali, si ikulu, ni ya bilionea mmoja aitwaye Ira Rennert.

Moja ya sehemu ya ndani

Jumba hili kubwa lina ulinzi mkubwa, si lazima kila mgeni anayeingia ndani ya jumba hilo apitie getini bali wengine wanaweza wakapitia katika njia za chini (underground), kwa ndani kuna michoro iliyogharimu kiasi cha dola milioni 500 ambazo ni zaidi ya trilioni moja, lina madirisha ya vioo visivyovunjika, kamera za CCTV, hata geti kubwa la kuingiliwa huwa limeunganishwa na umeme hivyo ni vigumu kwa wezi kuingia kizembe.

Na: Nyemo Chilongani, GPL

Leave A Reply