Hii Ndiyo Siri Mastaa wa Kike Bongo Kuibuka na Pub

MASTAA wengi wa filamu za Kibongo wameibuka na Pub ili kujipatia kipato cha upande mwingine ili kikidhi mahitaji yao wenyewe tofauti na zamani ambapo mbali na filamu walikuwa wakiwategemea wanaume wanaoingia nao kwenye uhusiano.

 

Ukiangalia kwa harakaharaka unaweza kusema mastaa hawa wameibukia hivi karibuni baada ya Uwoya kuibuka na Pub yake ya Last Minutes, lakini ukweli unabaki kuwa ni toka mwanzo kila walipojaribu kutoka kwa njia nyingine waliamua kuanzisha Pub huku wengine wakianzisha mapishi ya chakula.

 

Ukiacha Uwoya ambaye ni mgeni kwenye masuala ya Pub, miongoni mwa mastaa waliowahi kuwa na Pub toka kitambo ni pamoja na Aunt Ezekiel, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ Blandina Chagula ‘Johari’, Lungi Maulanga, Isabela Mpanda, Aunt Lulu nk.

 

Mastaa hawa wote waliwahi kumiliki Pub ambazo zilikuwa maeneo ya Kinondoni ambapo enzi hizo palisifika kwa mauzo ya vinywaji vya baa, ukiachana na Johari ambaye yeye alikuwa na Pub Sinza na sasa amejikita kwenye mapishi ya chakula tu kwa oda.

SIRI KUIBUKIA PUB KWA KASI HII

Baada ya kuwa na Pub huko nyuma na kuachana nazo, kwa sasa wameibuka upya ambapo alianza Uwoya, akaja Shilole, akamalizia Aunt ambaye wikienda iliyopita naye alizindua Pub kubwa yenye hadhi ya The Luxe.

 

Sababu ya kuibuka upya huenda kuna siri yao wenyewe wanayoijua lakini kubwa ni kuwaingizia fedha kwa haraka sana na nyingine zinazotajwa ni wateja wao wakubwa ni mashabiki zao ambao hufika kwa ajili ya kuwaona wao binafsi ambapo kuwaona kwa njia nyingine huwa ni vigumu.

 

“Hamjui tu ni kwa nini mastaa wanapenda kuibuka na biashara ya Pub, huko wanawapata mashabiki wao kirahisi na hasa hawa wenye fedha zao asikwambie mtu. “Ujue siyo rahisi kupata namba zao lakini wakienda Pub wanawapata na kwa sababu ya biashara hiyo hujikuta wanaongeza kipato zaidi,” alisema Lungi ambaye amewahi kumiliki Pub na kujiingizia kipato kikubwa.

 

Aliongeza kuwa, anakumbuka siku moja waliwahi kujipatia pesa ndefu kwa sababu wateja wengi walikuwa wakitaka kuhudumiwa na yeye mwenyewe kitendo ambacho kilikuwa ni fursa kwake kumuongezea dau kubwa.

MSIKIE MWINGINE ANAYEMILIKI PUB

“Mastaa kwa sasa wameamua kushindana kufungua Pub za kisasa ili kuwavutia wateja lakini yote hii ni kuigana tu huwa hawabuni vitu vipya vya kwao, mtu akiona mwenzake anapata pesa hapa naye anaingia,” alisema msanii mwingine.

 

Kuthibitisha hilo, mwandishi wa makala haya alifanya baadhi ya mahojiano na mastaa ambapo walifunguka kuwa siku kuna ushindani mkubwa na wengi wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha wanaingiza fedha.

“Unajua mastaa wanapenda kuigana sana na ndiyo maana hata akikuona unabwana flani atataka na yeye ahakikishe amempata ili tu apate pesa, sasa naweza kusema kuwa kwenye baa kunalipa asikwambie mtu ndiyo maana wamehamia huko kwani kwenye nguo wala saluni hakuna hela kwa sasa,” alisema Bela naye anamiliki Pub huko Mbezi Beach jijini Dar.

 

Aidha aliongeza kuwa kwenye baa kuna pesa za bwerere kutoka kwa mapedeshee ambao hupendelea starehe. “Kule kunalipa bwana asikwambie mtu mapedeshee wengi wanapenda starehe kwa hiyo bila shaka akitokea kwenye Pub yako ukampatia unamkamua kiulainii,” alisema Bela.

MASTAA WA KIKE WANAOMILIKI PUB

Ukiachana na walioacha kama vile Johari na Lungi, mastaa waliobaki kwenye ‘kilele’ na wanajipatia pesa kupitia Pub ni pamoja na Irene Uwoya, Isabela Mpanda, Shilole pamoja na Aunt Ezekiel ambaye amewaziba mdomo wote kwani ameingia kwa mara ya nne akiwa amejipanga zaidi ambapo mara ya kwanza alianzia Kindondoni ambapo alikuwa akiuza na aliyekuwa mpenzi wake Silva, akahamia na Demonte Mwananyamala kisha Kinondoni na sasa ni Mikocheni.


Loading...

Toa comment