The House of Favourite Newspapers

Hillary Clinton Augua Homa ya Mapafu, Aondolewa Kwenye Kumbukumbu ya Septemba 11

12campaign2-master675Mgombea Urais kutoka Chama cha Democratic, Hillary Clinton amegundulika kuwa na ugonjwa wa homa ya mapafu (pneumonia) baada ya kuugua ghafla jana Jumapili katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la Septemba 11 nchini Marekani.

Daktari wake Lisa Bardack amesema kuwa Bi Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa na kuongeza kuwa, Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio hilo la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la Al-Qaeda lililotokea Tuesday, Septemba 11, 2001.

Maelfu ya watu walikusanyika eneo la Ground Zero huko New York wakiadhimisha miaka miaka 15 tangu kundi la kigaidi la Al-Qaeda lililokuwa linaongozwa na Osama Bin Laden, kwa kuipua majengo mawili marefu zaidi duniani ambapo ni Makao Makuu ya Jeshi la Marekani, Pentagon na kuuwa watu 2,996 huku wakijeruhiwa watu 6,000 na kusababisha hasara ya jumla ya dola trilioni 3.

Baada ya hali hiyo kuokea ghafla, Clinton alilazimika kuondoka mapema, picha zilizowekwa mtandaoni zinamuonesha akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini baadae bi clinton alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri.

Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake.

Katika shughuli hiyo majina karibu 3000 ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa.

Comments are closed.