The House of Favourite Newspapers

Hip Hop, Singeli Kubamba Pasaka Hii Dar Live

 

Na MWANDISHI WETU| GAZETI LA AMANI| SHOW BIZ XTRA

KUONESHA kuwa mashabiki wengi wa burudani hususan wa Dar es Salaam wanapata kinachostahili, Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem unatarajia kuwashusha wakali kibao wa Muziki wa Singeli na Hip Hop Bongo, Pasaka hii.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mbali na wakali wengi wa Hip Hop na Singeli Bongo kutamba , siku hiyo pia kutakuwa na wakali wa ndondi pamoja na Muziki wa Taarab.

“Niwagusie tu, Pasaka hii itakuwa ya kitofauti kutokana na uwepo wa wakali kila kona, kinachotakiwa kufanyika ni kutega sikio redioni na kufuatilia Magazeti ya Global Publishers ili ujue listi kamili ya wakali watakaokuwepo kuanzia, Taarab, Hip Hop, Ndondi pamoja na Singeli,” alisema Mbizo. Mbizo alimalizia kuwa michezo ya watoto nayo itakuwepo kuanzia asubuhi.

 

Comments are closed.