The House of Favourite Newspapers

Historia Imeandikwa Kwenye Tuzo za EATV Mlimani City

 eatv-26Host wa tuzo za EATV 2016, Salama Jabir akifanya yake usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar.

eatv-27Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (kulia) akijiandaa kumtaja Muigizaji Bora wa Kiume.

eatv-29

Lulu akimtaja Muigizaji Bora wa Kiume, Salim Ahmed (Gabo) hayupo pichani.

eatv-31Staa wa filamu Bongo, Gabo (wa pili kutoka kushoto) akikabidhiwa tuzo yake.

eatv-32Gabo akiongea neno baada ya kuibuka Muigizaji Bora wa Kiume.

eatv-1

Mshindi wa tuzo tatu za EATV 2016 katika vipengele vya Video Bora ya Mwaka, Wimbo Bora wa Mwaka na Mwanamuziki Bora wa Kiume, Ali Kiba ‘King Kiba’ akijiweka sawa kwenda kuchukua tuzo yake ya Video Bora ya Mwaka.

eatv-2

Ali Kiba ‘King Kiba’  akipokea tuzo ya Video Bora ya Mwaka.

eatv-4

Ali kiba akiongea na mashabiki wake.

eatv-6

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akiwa katika Usiku wa Tuzo za EATV Mlimani City.

eatv-9

Ali Kiba akipokea tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume.

eatv-10

…Akiongea na mashabiki wake baada ya  kupewa tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume.

eatv-5

Ali Kiba akimkabidhi mdogo wake Abdul Kiba tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume.

eatv-11

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Juma Jux ‘Jux’ akiwa kwenye pozi na mpenzi wake Vanessa Mdee ‘Vee Money’ .

eatv-12

Mashabiki mbalimbali wakiendelea kufuatilia utoaji tuzo hizo.

  eatv-14

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto)  akimsikiliza Bonny Love mshindi wa tuzo ya heshima.

eatv-16

Lady Jaydee ‘Jide’ aliyeibuka mshindi wa tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike akimkabidhi tuzo  mpenzi wake Rasta.

eatv-17

Lady Jaydee ‘Jide’ akiondoka na Rasta wake wakiwa wamekumbatiana.

eatv-20

Nape Moses Nnauye (kulia) akiwapongeza washindi wa tuzo za EATV 2016 .

Historia imeandikwa kwenye tasnia ya sanaa nchini ambapo kwa mara ya kwanza tukio la utoaji wa tuzo za EATV  kwa wasanii wa muziki na filamu Afrika Mashariki, limefanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo, mmgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Moses Nnauye.

Tuzo hizo  ziliandaliwa na East Africa Television (EATV) Ltd, zikilenga kuboresha kazi za sekta ya sanaa, zinatolewa kwa wasanii mbalimbali wanaojihusisha na sanaa katika kutambua mchango wao pamoja na ubora wa kazi zao.

Lengo la kuanzisha Tuzo za EATV ni katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo na ushindani katika Sekta ya Sanaa Afrika Mashariki ili kusaidia kuziboresha viwango vyake na kuwa na kazi nzuri zenye ubora unaoweza kushindanishwa kimataifa.

Tazama orodha nzima ya washindi hapa chini..

MWANAMUZIKI BORA CHIPUKIZI
Feza Kessy
Mayunga Nalimi (Mayunga)
Amani Hamisi (Man Fongo) – Mshindi
Rashid Said (Bright)
Rukia Jumbe (Rucky Beby)

KUNDI BORA LA MWAKA
Navy Kenzo – Mshindi
Mashauzi Classic
Team Mistari (Kenya)
Sauti Sol (Kenya)
Wakali Wao

MUIGIZAJI BORA WA KIKE
Chuchu Hansy – Mshindi
Rachel Bithulo
Frida Kajala Masanja
Khadija Ally

MUIGIZAJI BORA WA KIUME
Meya Shabani Hamisi
Salim Ahmed (Gabo) – Mshindi
Daudi Michael (Duma)
Dotto Hussein Matotola
Saidi Mkukila
VIDEO BORA YA MWAKA
Namjua – Shetta
Njogereza – Navio
Aje – Ali Kiba – Mshindi
Don’t Bother – Joh Makini
NdiNdiNdi – Lady Jay Dee

WIMBO BORA WA MWAKA

Don’t Bother – Joh Makini
NdiNdiNdi – Lady JayDee
Kamatia Chini – Navy Kenzo
Aje – Alikiba – Mshindi
Moyo Mashine – Ben Pol
FILAMU BORA YA MWAKA
Facebook Profile
Safari ya Gwalu – Mshindi
Mfadhili Wangu
Hii ni Laana
Nimekosea Wapi
MWANAMUZIKI BORA WA KIKE
Lilian Mbabazi (Uganda)
Ruby
Lady Jay Dee – Mshindi
Linah
Vanessa Mdee

TUZO YA HESHIMA KACHUKUA BONNY LOVE

MWANAMUZIKI BORA WA KIUME
Gnako
Shetta
Mwana FA
Ben Pol
Alikiba – Mshindi

(PICHA: RICHARD BUKOS/GPL)

Comments are closed.