The House of Favourite Newspapers

ROMA: Historia Itaandikwa Dar Live Idd Mosi

0
Roma Mkatoliki akikinukisha

NAJUA hukuijua hii! Huku sakata lake la kutekwa likiwa limemalizwa kiaina, staa wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ kwa mara ya kwanza sikukuu hii ya Idd Mosi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani,Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar, ataweka kila kitu ‘A-Z’ kutekwa kwake sambamba na kukamua shoo la kihistoria akisindikizwa na wakali kibao wa michano.

Umemisi ile michano yake? Umemisi ile amshaamsha popo yake, basi usijali! Tangu kuanza kwa mwaka huu, staa huyo hajawahi kufanya shoo yoyote lakini kwa mara ya kwanza atashuka Sikukuu ya Iddi Mosi Dar Live na kukinukisha kwa ngoma zake zote kali zilizowahi kutamba na zile ambazo mpaka leo hii zinaendelea kuwa gumzo kila kona ya jiji ikiwemo K, Kaa Tayari, Tanzania, Viva Roma Viva na nyingine kibao.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo amesema kwamba ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kwa nguli huyu kukinukisha kabla la sekeseke la kutekwa kwake ilikuwa Mkesha wa Mwaka Mpya uliofanyika Dar Live na kwa sababu anataka kukutana na mashabiki wake ambao walimpa sapoti kabla ya kutekwa, ameamua kufungua burudani katika uwanja huohuo unaotikisa kwa kutoka burudani kabambe Bongo.

Mr. Blue akifanya yake

Wakali kibao kumpa kampani

Huku ukiwa unakamilishwa usiku wa kihistoria ndani ya Dar Live, R.O.M.A hatakuwa peke yake bali atasindikizwa na wakali wa michano kibao akiwemo Mr. Blue ‘Byser’, Stamina, Darassa pamoja na mkali wa kuruka na vyura, Snura bila kulisahau Kundi la Muziki wa Taarab la Zanzibar Stars.

Kuanika A-Z kutekwa kwake

Kama ulikuwa hujui sasa ngoja nikuchane! Mkali huyu wa michano atapanda jukwaani na kusimulia mchongo mzima wa kutekwa kwake A-Z, ilikuwaje? Alipelekwa wapi na ilikuwaje mpaka akaachiwa? Majibu yote ya maswali hayo utayapata Sikukuu ya Idd Mosi ndani ya kiwanja cha wajanja, Dar Live.

Nishushe Idd Mosi… Roma Atawaongoza Wakali Hawa Kuliamsha Dude, Dar Live


Bofya hapa kumsikia

Huku akionekana kuwa na mzuka wa kuchana jukwaani, R.O.M.A amesema kwamba siku hiyo itakuwa balaa, atachana kama hakuwahi kuchana kabla, atawaonyeshea watu jinsi michano ya kweli inavyofanywa na namna ambavyo jukwaa linatakiwa kutawaliwa.

“Utakuwa ni usiku wa kibabe! Sipendi kukosea, sipendi watu wajute kwa nini wamekuja kumcheki R.O.M.A. Nitafanya vitu ambavyo watu hawajawahi kuviona hata kwa wasanii wa mbele. Ukitaka kuona ni kwa namna gani kutekwa kwangu kumenipa mzuka, wewe ibuka Dar Live ujionee na usikie kila kitu kutoka kwangu.”

Bambo, Wakali Dancers ndani

Ili kuwafanya watu wa rika zote siku hiyo waburudike, uongozi wa Dar Live umesema kuwa msanii wa vichekesho kutoka Kundi la Ze Komedy,

Bambo atakuwepo mapema kuanzia saa 2:00 asubuhi kwa lengo moja tu la kuwaburudisha watoto lakini pia kundi la sarakasi na kudensi, Wakali Dancers watakuwepo kutoa burudani huku nao Kundi la Muziki wa Asili la Makhirikhiri kutoka Tanzania likisimamia shoo nzima ya watoto.

Mbali na uwepo wa wakali hao, watoto pia watapata kuburudika na michezo ya kubembea, kucheza kwenye treni na ndege, kuogelea na mingine kibao vyote hivyo kwa kiingilio kiduchu tu cha shilingi 3,000 tu getini.

Unakosaje kwa mfano?

Vuta picha umepiga mzigo wa maana, mishe kibao, umejichanga mwezi mzima, umekamata fuba la maana, kwa nini usimsindikize R.O.M.A jukwaani huku ikiwa ni wiki chache baada ya kuachwa huru kule alipotekwa? Kwa mchongo wa shilingi 7,000 tu unazama bila ubishi wowote ule kuanzia saa 2:00 za usiku mpaka jogoo aseme inatosha.

NA MWANDISHI WETU : IJUMAA WIKIENDA | OVER ZE WEEKENDA

 

R.O.M.A Mkatoliki Alivyorudi Darasani Kufundisha Somo la Hisabati

Leave A Reply