The House of Favourite Newspapers

HIVI NDIVYO AMBER LULU ALIVYONUSURIKA AJALINI

Lulu Eugen ‘Amber Lulu’

MSANII wa Bongo Fleva, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ ameponea chupuchupu baada ya kupata ajali ya gari na kutoka salama licha ya kupata jeraha dogo mkononi.  

 

Msanii huyo aliiambia Star Showbiz kuwa, anamshukuru Mungu kwa kuwa ametoka salama kwenye ajali hiyo iliyotokea juzikati usiku wakiwa njiani kuelekea katika siku ya kuzaliwa ya msanii mwenzao, Messen Selekta.

 

“Kwa kweli ilikuwa ajali mbaya sana, kwa sababu hata ukiiangalia gari tuliyokuwa tumepanda huwezi kuamini kama kuna watu wamepona, imeharibika vibaya, namshukuru sana Mungu kwa sababu nimetoka salama japo nina jeraha dogo mkononi,” alisema Amber Lulu.

MEMORISE RICHARD

Comments are closed.