Hivi Ndivyo Dili la Makusu, Yanga Lilipofika

HATIMAYE dili la mshambuliaji Jean Marc Makusu kutua Yanga limeingiwa na doa mara baada ya uongozi wa timu hiyo kugundua kuwa mshambuliaji huyo kuwa na majerahaya mara kwa mara.


Hapo awali uongozi wa Yanga ulikuwa katika
mpango wa kumsajili Makusu kwa ajili ya kuja kuongoza nguvu katika eneo la ushambuliaji ya timu hiyo ambapo kwa sasa linachezwa na Fiston Mayele na Heritier Makambo.


Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimeliambia
Championi Jumamosi, kuwa uongozi wa Yanga umeamua kuachana na Makusu kutokana na mshambuliaji huyo kuwa na majeraha ya mara kwa mara mara baada ya kuwahi kuvunjika mguu wake wa kushoto kipindi ambacho yupo Orlando Pirates ya Afrika Kusini.


“Uongozi wa Yanga umeona ni busara kwao
kuachana na usajili wa Makusu kutokana na majeraha ambayo amekuwa akipata mara kwa mara baada ya kuwahi kuvunjika mguu alipokuwa akikipiga Orlando Pitares.


“Tangu avunjike mguu wake wa kushoto na
alipopona bado alikuwa akipata majeraha ya mara kwa mara tofauti na alipokuwa AS Vita ambao alikuwa yupo fiti na alikuwa anacheza kwa kiwango kikubwa sana, hivyo ni ngumu
tena kwake kusajiliwa na Yanga mara baada ya
kugundua hilo,” kiliweka wazi chanzo hicho.


Champioi Jumamosi lilimsaka Makusu
mwenyewe ambapo alifunguka: “Kila kitu kuhusu usajili wangu uongozi wangu ndio unahusika, mambo ya usajili huwa yana mambo mengi kwangu nacheza mpira kisha uongozi unatenda zaidi juu ya usimamizi wangu.”

STORI: MARCO MZUMBE NA RICHARD NGAILA, Dar es Salaam3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment