The House of Favourite Newspapers

HIVI NDIVYO… MASTAA WANAVYOFURAHIA VALENTINE’S DAY

SIKU ya Wapendanao (Valentine’s Day) ni siku inayoaminiwa duniani kote kuwa ni maalum kwa mtu unayempenda.

Hata hivyo, siku zilivyozidi kusonga ikawa siyo maalum kwa wapenzi tu, hata kwa marafiki na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.

Leo ndiyo siku yenyewe ambapo Gazeti la Amani limefanya mahojiano na mastaa mbalimbali Bongo.

Mastaa hao wanazungumzia siku hii itakuwaje? Watakuwa na nani na yupi ambaye atakuwa ‘Valentine’ wao. Wamefunguka kama ifuatavyo;

WEMA ISAAC SEPETU

Staa huyu kwa muda mrefu, baada ya kuachana na mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ hajawahi kuwa na uhusiano maalum na mtu au kudumu naye kama mpenzi hivyo kwa upande wake anasema Valentine wake ni mama yake kwa sababu ndiye anaamini ni mtu pekee anayempenda hapa duniani.

“Mtu wangu ambaye ni maalum na nitakuwa naye Valentine ni mama yangu mzazi (Mariam Sepetu). Ndiye ninayempenda sana kwa sababu sijaona mwingine na wala sidhani kama kuna mwanaume anayeweza kuchukua nafasi ya mama yangu kwa sasa. Ninaweka wazi kuwa ninampenda sana,” anafunguka Wema.

KULWA KIKUMBA ‘DUDE’

Mwigizaji huyu ambaye alitamba na kundi lake la Bongo Dar es Salaam alifunguka kuwa kwa upande wake, Valentine wake ni mkewe ambaye naye alikuwa ni msanii. Anasema hii ni kwa sababu ni mke mwema na amemzalia watoto wazuri sana.

“Nani anaweza kuwa Valentine wangu zaidi ya mke wangu na pembeni ikawa familia yangu ninayoipenda? Maana japokuwa sisi tunapendana siku zote, lakini siku hii kwa mke wangu itakuwa maalum sana,” anasema Dude.

ESTER KIAMA

Mwigizaji huyu wa filamu za Kibongo, hajawahi kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi wa moja kwa moja, lakini anasema siku ya leo ni maalum kwa yeye na familia yake. Anasema anapozungumzia familia anajumuisha na mtu anayempenda pia.

“Siku ya leo nitakuwa na familia yangu na nikisema familia ni pamoja na mtu ninayempenda ndani yake. Hivyo nitakuwa bize na watu wangu wa karibu sana ambao wanazunguka kila siku kwenye maisha yangu,” alieleza Ester.

FAIZA ALLY

Faiza ni mwigizaji ambaye ana vituko vingi sana. Ameifungukia Valentine yake leo kuwa, kwa kuwa mpenzi wake yuko mbali haijalishi kuwa atashindwa kumuonesha anampenda, lakini siku yake ya Wapendanao ataimalizia kwa watoto wake ambao anaona ndiyo kila kitu kwenye maisha yake.

“Ninampenda baba Li, lakini yupo mbali sasa, salamu zangu za upendo atazipata tu ila nina wapenzi wangu wawili ambao ni watoto wangu. Kwa kweli hao ndiyo nitasherehekea nao kwa sababu ninawapenda sana,” anafunguka Faiza.

AUNT EZEKIEL

Aunt ambaye ni staa wa Bongo Muvi anajulikana kabisa mpenzi wake ni dansa wa Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo. Tayari wamezaa mtoto mmoja wa kike, lakini ameweka wazi mtu wake ambaye atamuonesha upendo wote ni mtoto wake na si mtu mwingine.

“Valentine wangu ni Cookie (mtoto wake), yaani huyo ndiye naamini kuwa ananipenda sana na upendo wake kwangu hauwezi kubadilika hata siku moja hadi ninazeeka. Yeye ndiye naweza kumpeleka sehemu nzuri, akafurahi,” anasema Aunt.

IRENE UWOYA

Staa huyu Bongo Muvi ambaye bado anaumiza vichwa vya wengi juu ya ni nani mpenzi wake kwa sasa baada kuachana na msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ amefunguka kuwa yeye katika siku hii atakuwa na mtu anaye

mpenda hivyo watu wajue hivyo kwa sababu kama mwanadamu, hawezi kuishi bila mpenzi.

“Nitakuwa na mpenzi wangu. Waliobahatika kumjua wanamjua, wasiobahatika ndiyo hivyo, ila nitakuwa na mtu ninayempenda sana,” anafuguka Uwoya.

KAJALA MASANJA

Mwanamama huyu wa Bongo Muvi ambaye uhusiano wake wa wazi ulikuwa zamani alipokuwa na mzazi mwenzake, Paul Matthysse ‘P Funky’, lakini tangu kipindi hicho hajawahi kuonesha mpenzi wake hadharani, yeye anasema Valentine wake ni mtoto wake (Paula) ingawa mpenzi wake yupo.

“Mtu ambaye naweza nikawa naye na kukiri ninampenda zaidi ni mtoto wangu (Paula), lakini simaanishi kuwa sina mtu ila kama kuwa na watu ninaowapenda Valentine (leo) ni hao wawili,” anaeleza Kajala.

ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’

Mwanamuziki huyu wa mduara yeye kwa sasa yuko kwenye ndoa na Ashraf Uchebe. Shilole anasema kuwa siku yake ya leo atakuwa na mume wake huyo kipenzi na si mtu mwingine yeyote, ingawa kwa upande wao kila siku ni Valentine.

“Mume wangu ndiye Valentine wangu wa ukweli na sisi kwetu Valentine ipo kila siku ila kwa siku hii muhimu inatakiwa aone kitu tofauti kidogo,” anafunguka Shilole.

Makala: Imelda Mtema.

BELLA Amlipua DIAMOND Ishu ya DIMPOZ, “Hawajapost Wimbo Wake”

Comments are closed.