The House of Favourite Newspapers

Hivi ndivyo x-rays zinavyoua watanzania

0

Na Mwandishi Wetu

LICHA ya upigaji X-rays kuwa muhimu katika matibabu ya binadamu, lakini upande wa pili zina madhara yanayotokana na mionzi ya kifaa hicho.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, X-rays zina madhara makubwa hususan kwa akina mama wajawazito.

Mara nyingi tumeona watu wakipimwa kwa X-rays kutokana na kuumia sehemu mbalimbali mwilini kama vile mifupa na misuli kama kuteguka kwa ‘enka’ au maeneo mengine lakini kitu kibaya kinachotokana na matumizi ya mashine hizo ni wengi wanaozitumia hawapati ushauri wa kitaalam kutoka kwa wahusika na hawaelewi madhara makubwa yatokanayo na mashine hizo.

Kwa hapa nchini, baadhi ya madaktari, hususan wa hospitali za binafsi, wamekuwa wakifanya upimaji wa X-rays kama biashara, hivyo mgonjwa anapokwenda hospitali, daktari humshauri kufanya vipimo vya X-rays hata kama tatizo alilonalo halihitaji kipimo hicho.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Ener-Chi Wellness Centre, watu hupata madhara zaidi wanapofanyiwa kipimo hicho kwa mara ya kwanza, hivyo kuepuka tatizo bora kutotumia kama hakuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Wataalam wanaeleza kuwa, madhara yatokanayo na mionzi ni hatari zaidi kwa watoto kuliko watu wazima.

Kutokana na maumbile yao kuwa madogo, ni rahisi kwao kupata madhara makubwa ya mionzi mwilini ikiwa ni pamoja na kuathirika sehemu za uzazi. Wazazi wanaofuatana na watoto wao kwenda kufanya X-ray, nao wanashauriwa kuvaa nguo za kuzuia mionzi hiyo kama tahadhari.

Kwa mjamzito, mionzi ya X-ray ina uwezekano wa asilimia 40 kuathiri kiumbe kilichopo tumboni kwa kupata kansa. Upo pia uwezekano wa asilimia 50 kusababisha mtoto apate vimbe mwilini na asilimia 70 kukabiliwa na upungufu wa damu.

Bahati mbaya sana, wapo baadhi ya madaktari ambao wamekuwa wakiwataka wajawazito kupiga X-ray bila kujua ni kiasi gani mionzi inakwenda kumuathiri mtoto tumboni. Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply