Hivi ni Kweli Faiza Amekata Ringi?

Faiza Ally.

FAIZA bhana! Ukimfikiria unaweza usimmalize kutokana na vituko ambavyo amekuwa akifanya kwenye mtandao wa Instagram.

 

Amekwishawahi kuposti picha wakati akiwa leba anajifungua na hivi karibuni amewaacha watu midomo wazi baada ya kuposti video akiwa ameshika nguo ya ndani ‘kabati’ iliyotoboka na kufunguka kwamba inamkumbusha mbali kwenye ulimwengu wa mapenzi, haaa haaa! Hata hivyo, baada ya video ile, naye alichezea matusi huku wafuasi wengi wakimnanga kwenye komenti kwamba amekata ringi, kwa maana kwamba hana heshima wala adabu na haoni jambo la aibu hata kujidhalilisha mwenyewe!

 

Dishi Bovu liliamua kumsaka kuzungumzia posti zake hizo na mtazamo ambao jamii inauweka kwake; Dishi Bovu: Faiza mumy!

 

Faiza: Mambooo!

 

Dishi Bovu: Kwangu salama tu! Nilikuwa naulizia lile kufuli uliyoposti… hivi ulifikiria nini mama?

 

Faiza: Nafanya ninachokipenda, siwezi kuacha kufanya jambo kwa sababu ninaogopa watu watanitazamaje!

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment