visa

#GlobalCars: Hizi Ndio Ndinga 10 Kali Zilizoshine Zaidi Kwenye Movie Ya Fast & Furious 8 – (Pichaz)

Kwa wale wadau wangu wa kuroll mtaani ‘in everything nice rimz’ basi naamini moja ya vitu vilivyotrend zaidi kwenu kwenye franchise movie ya Fast & Furious 8 ni pamoja na aina tofauti ya magari yanayoonekana kwenye movie hiyo.

Ukiachana na majina makubwa kama Lamborghini, Bugatti, Ferrari, Rolls Royce na pengine Bentley, binafsi siyajui sana magari lakini tukiyazungumzia kwa ujumla na kwa ufahari wao huwezi kuacha kutaja aina tofauti ya magari yanayoonekana kwenye movie zote za Fast & Furious. Ni noma! 

So, kwa wale ‘petrol heads’ wangu hii ni kwa ajili yenu, nimekusanya picha 10 za ndinga kali zilizoshine zaidi (kwenye scene tofauti) kwenye Fate Of The Furious na kukuwekea hapa chini. 

Ziperuz and enoy!

01. Rally Fighter.

Gari hii imeendeshwa na Letty Ortiz (Michelle Rodriguez) 

02. Orange Lamborghini

Kwenye movie, gari hii imeendeshwa na Roman (Tyrese Gibson)

03. Bentley Continental.

Imeendeshwa na  Dom (Vin Diesel).

04. 1966 Chevrolet Corvette Stingray 

Imeendeshwa na Letty Ortiz (Michelle Rodriguez)

05. Mercedes AMG GT.

Mmiliki wa hii gari alikuwa ni Tej Parker (Ludacris)

06. Dodge Ice Charger.

Na hii nayo iliendeshwa na Dom (Vin Diesel).

07. Ripsaw 

Kwa mara nyingine tena Tej Parker (Ludacris) alionekana ndani ya hii mashine.

08. Ice Ram

Mashine ya kibabe kwa ‘Hobbs’ mtu wa kibabe (The Rock)

09. Subaru BR-Z

10. Jaguar F-TYPE COUPE:

Hii imeendeshwa na Deckard Shaw (Jason Statham)

Kwa wale ambao bado hawajaicheki Fast & Furious 8, bado hamjachelewa screening ya movie hii bado inaendelea kwa wiki hii kwenye kumbi za sinema za Mlimani City kwenye mida ya: 1:45 Mchana, 4:30 Jioni, 6:45 Jioni, 7:15 Usiku, 9:30 Usiku pamoja na Saa Nne kamili usiku.

Kama umeshaicheki Fast & Furious 8,  tumia uwanja wa comments kuniambia ni gari gani ilibang zaidi kwako na kwanini.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Pichaz: Google.
Toa comment