The House of Favourite Newspapers

Hizi Ndizo Sababu za Upungufu wa Nguvu Za Kiume… Dokta atoa Ushauri Huu

0

Kwa kawaida mwanaume ili uume uweze kufanya kazi uhitaji ushirikiano wa mifumo minne.

Kwanza ni mfumo wa mishipa ya damu ambao huingiza damu katika uume, mfumo wa neva za fahamu ambao hutoa taarifa kutoka kwenye ubongo hadi kwenye uume na kurudisha taarifa kutoka kwenye uume kwenda kwenye ubongo.

Pia, kuna mfumo wa homoni na vichocheo vya mwili vinavyohitajika kuchochea mishipa ya damu kutanuka ili uume ufanye kazi na mfumo wa akili na saikolojia.

Kwa kawaida; uwezo wa ufanyaji kazi wa viungo vya uzazi vya mwanaume hupungua kadri umri unavyokwenda.

Kwa ujumla tafiti zinaonyesha kwa kila wanaume 100 wenye umri wa miaka 20 hadi 75, changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume huathiri wanaume 16.

Kiwango huwa kikubwa kwa wazee , kwa wastani wa asilimia 37 ya wazee wenye miaka 70 hadi 75 wanakabiliwa na tatizo hili.

Changomoto kubwa iliyopo sasa ni kwamba baadhi ya wanaume wanapoona uwezo wao utendaji kazi wa uume umepungua huamua kujinunulia dawa kama viagra au za asili bila kufahamu chanzo cha tatizo.

Tafiti zinaonyesha upungufu wa nguvu za kiume huweza kuwa kiashiria cha tatizo la kiafya linaloendelea ndani ya mwili.

Chanzo cha upungufu nguvu za kiume

Kwa mfano: tafiti za magonjwa ya mfumo wa mishipa ya damu, magonjwa ya moyo na kisukari zimeonyesha kuwa kuna uhusiano wa upungufu wa nguvu za kiume na uwepo wa magonjwa haya.

Vivyohivyo upungufu wa nguvu za kiume unapotokea huweza kuwa kiashiria za ukubwa wa matatizo yanayoathiri mfumo wa mishipa ya damu, moyo na neva za fahamu.

Tafiti zinaonyesha kwa kila wanaume 100 wenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, 90 kati yao tatizo hili huwa limetokana na magonjwa mengine ya kimwili na 10 hutokana na matatizo ya kisaikolojia.

Hivyo ni muhimu kwa mtu mwenye tatizo kufanyiwa uchunguzi hospitalini kujua kama ana magonjwa mengine ya kiafya na kupatiwa tiba stahiki sio kunywa dawa za kuongeza nguvu kiholela bila kujua chanzo.

Takribani asilimia 70 ya wanaume wenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume; tafiti zinaonyesha huwa tatizo linatokana na magonjwa ya mishipa ya damu.

Matatizo haya yanajumuisha ugonjwa wa kurundikana kwa lehemu kwenye kuta za mishipa ya damu, ugonjwa wa shinikizo kubwa la damu.

Magonjwa haya huathiri namna damu inayopita ndani ya mishipa na kufanya uume usiweze kutenda kazi vyema. Matatizo haya mara nyingi hukumba watu wenye umri mkubwa hasa zaidi ya miaka 60.

Pia, upungufu wa nguvu za kiume umehusishwa na kuwa kiashiria cha kuongezeka uwezekano wa kupata kiharusi au shambulio la moyo.

Hivyo wagonjwa hutakiwa kuripoti wanapoona uwezo wa uume kusimama unapungua maana huweza kuwa kiashiria ugonjwa unakua.

Tatizo la kisukari pia, huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume. Kiwango cha sukari kisipodhibitiwa huharibu mishipa ya damu na neva za fahamu hivyo kufanya uume kuwa vigumu kusimama vyema.

Takwimu zinaonyesha takribani asilimia 35 hadi 50 ya wanaume wenye kisukari hupata kiasi fulani cha upungufu wa nguvu za kiume hasa ikiwa hawazingatii kanuni za kudhibiti sukari kwenye damu.

Magonjwa ya mfumo wa fahamu na neva huweza pia kusababisha upungufu wa nguvu za kiume. Magonjwa kama kiharusi, ugonjwa wa kupoteza ufahamu kama Alzeheimer, matatizo ya uti wa mgongo huathiri mawasiliano kati ya ubongo na uume hivyo kusababisha shida ya uume kusimama.

Pia, ugonjwa wa upungufu wa nguvu za kiume huweza kuchangiwa na matumizi ya baadhi ya dawa, majeraha kwenye uume, magonjwa ya figo, matumizi ya sigara, matumizi ya pombe kupita kiasi na upasuaji ndani ya eneo la nyonga.

Chanzo kingine ni matatizo ya kwenye afya ya akili kama sonona au ya kisaikolojia hasa woga.

USHAURI

Ni muhimu kwa wanaume ambao wanaokabiliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwenda hospitali ili wachunguzwe afya nzima kwa ujumla na kugundua matatizo mengine makubwa ya kiafya ambayo yameanza kuonyesha dalili kupungua nguvu za kiume, kuchunguza kama una ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu, ugonjwa wa figo, kisukari na shinikizo la damu.

Kugundulika tatizo kutasaidia wao kupatiwa tiba stahiki kulingana na kiwango cha tatizo.

Na DK. Chale SIMU: +255 713 350 084

EXCLUSIVE: SOPHIA wa “AMELOWA” AFICHUA UKWELI PENZI LAKE na HARMONIZE, KUMLIZA KAJALA | DSM FLAVOUR

Leave A Reply