The House of Favourite Newspapers

Homa ya Matumbo kwa Mtoto

0


UGONJWA wa homa ya matumbo kwa watoto, ni wa kawaida kwa watoto kutokana na aina ya michezo na uchafu wanaokula, hasa watoto wadogo. Hata hivyo, mtoto anapoharisha na kutapika, mzazi hatakiwi kupuuza kwa sababu yawezekana ni dalili ya ugonjwa mwingine mkubwa kwa sababu dalili za awali za magonjwa mengi ya watoto, huwa ni kuhara na kutapika.

Hatari kubwa ni kwamba, mtoto anapohara na kutapika, hupoteza maji mengi nakama mzazi akipuuzia, mtoto anaweza kupoteza maisha huku akimshuhudia ndiyo maana inasisitizwa kwamba mtoto anapohara na kutapika mfululizo, ni lazima wazazi wampeleke hospitali haraka iwezekanavyo.

Endapo wazazi wanaishi mbali na hospi tali, wanashauriwa kuwa na akiba ya dawa maalum ya ORS ambayo hutumiwa kuchanganya kwenye maji na kumnywesha mtoto ambaye amepoteza maji mengi kwa kuharisha na kutapika.

Mnyweshe mtoto mchanganyiko huu na kama kuna maziwa fresh, pia mtoto apewe wakati jitihada za kumpeleka hospitali zikifanyika. Dalili za mtoto aliyeishiwa maji kutokana na kuharisha, ya kwanza huwa ni macho kuingia ndani.

Pia mtoto kutotoa machozi anapolia, mdomo kukauka, kukojoa mkojo wa njano na kutoa kiwango kidogo cha mkojo. Unapoona dalili hizi, ujue hali ya mtoto imefi kia pabaya, wahi hospitali. Pia kwa kuwa magonjwa ya kuhara na kutapika huambukizwa kwa haraka kutoka mtoto mmoja kwenda mwingine, au wakati mwingine hata kwenda kwa mtu mzima, Gofu la bwawa la kuogelea.

Inapaswa wazazi wakadumisha usafi kila sehemu, ikiwa ni pamoja na kusafi sha haraka maeneo mtoto alipotapikia au kuharisha. Wanafamilia wote ambao wana mgonjwa wa kuhara, wanapaswa kunawa mikono kabla ya kula, tena kwa kutumia sabuni, kunawa mikono baada ya kutoka chooni, kuhakikisha watoto wanaoumwa hawajichanganyi na watoto wengine na taratibu nyingine za usafi .

Leave A Reply