The House of Favourite Newspapers

Home Shopping Centre nao kufunga maduka yao

0

home-shopping-center 2

Mojawapo ya maduka ya Home Shopping Centre.

Na Clarence Mulisa

KAMPUNI ya Home Shopping Centre nayo imetoa azimio la kutaka kusitisha huduma zake na kufunga maduka
kama walivyofanya wenzao wa Uchumi Supermarket hivi karibuni.

home

Katika notisi ya azimio iliyotolewa kwa umma na mfilisi Yusufu Mohamed wa Law Domain Advacates kwenye
gazeti la serikali la Daily News leo inaonyesha kuwa maazimio yaliyofikiwa Oktoba 5, mwaka huu, Home Shopping Centre Ltd ilikubali kwa hiari kufunga huduma zake.

Katika azimio hilo, Yusufu Mohamed ndiye aliyeteuliwa kuwa mfilisi kwa ajili ya kufunga huduma za kampuni hiyo.

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Mfilisi huyo amewataka wote wanaoidai kampuni hiyo kuleta vielelezo vinavyoonyesha madai yao kwake
ndani ya siku 14 tangu kutolewa kwa notisi hiyo iliyosainiwa Oktoba 15, mwaka huu.

Kwa hatua hiyo Kampuni ya Home Shopping Centre itakuwa imeungana na Uchumi Supermarket ambao wamefunga maduka yake Tanzania na Uganda baada ya kushindwa kutengeneza faida.

Leave A Reply