The House of Favourite Newspapers

Horoya Waitumia Yanga Mkataba Wa Makambo

0

MABOSI wa Yanga, jana Alhamisi walikuwa wana bashasha kwenye sura zao kutokana na kuwa wanasubiri majibu ya dili la straika Heritier Makambo kutoka kwa Horoya AC ya Guinea ambayo inammiliki mchezaji huyo.

 

Yanga walikuwa wanasubiri majibu hayo kutoka kwa Makambo baada ya hivi karibuni kumtumia mkataba lakini akashindwa kuusaini kutokana na kipengele cha kimkataba alichokuwa nacho na Horoya. Straika huyo Mkongomani aliyefunga mabao 17 kwenye Ligi Kuu Bara aliondoka Yanga na kutua Horoya AC na kusaini mkataba wa miaka mitatu.

 

Kwa sasa Yanga wanamhitaji Makambo kwa ajili ya kuitilia nguvu safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa msimu huu kinara wake wa mabao ni David Molinga mwenye nane.

 

Habari za ndani ambazo Championi Ijumaa, limezipata ni kuwa majibu hayo waliyokuwa wanayasubiri Yanga ni kutokana na Makambo kuomba kufanya maongezi na Horoya kwa ajili ya kukatisha mkataba wake.

“Unajua Makambo alitumiwa mkataba na Yanga kwa ajili ya kusaini na kuangalia vitu vingine ikiwemo maslahi yake, lakini ilikuwa ngumu kusaini kwa sababu ya mkataba wake na Horoya.

 

“Kwa hiyo kilichofanyika ni yeye na wakala wake kuzungumza kwanza na klabu yake hiyo ya sasa kwa ajili ya kumalizana nao kutokana na kusaini miaka mitatu na mazungumzo hayo majibu yake yalikuwa yanakuja jana Alhamisi.

 

“Kwa hiyo viongozi walikuwa wakisubiri majibu hayo kwa ajili ya kumalizana naye moja kwa moja,” kilisema chanzo hicho. Upande wa Yanga, Ofi sa Mhamasishaji, Antonio Nugaz amesema: “Kitu cha msingi ni kuomba Mungu tu kwani Yanga ya msimu ujao itakuwa ya tofauti sana.”

STORI NA MUSA MATEJA NA SAID ALLY – CHAMPIONI IJUMAA

Leave A Reply