The House of Favourite Newspapers

Hospitali ya Kijitonyama Yaishukuru Meridianbet kwa Msaada

Wakali wa ubashiri Tanzania nzima, imeendelea kuonesha moyo wa kujali jamii kwa kutoa msaada wa mashuka kwa Hospitali ya Kijitonyama, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kusaidia sekta ya afya nchini Tanzania.

Msaada huo unalenga kuboresha huduma za afya kwa wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo kwa kuwapatia mazingira safi na salama. Mashuka yaliyotolewa yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha kwamba wagonjwa wanapata huduma bora wakiwa kwenye mazingira yenye usafi unaozingatiwa.

Baada ya kutoa msaada huo wa mashuka, Nancy Ingram ambaye ndiye aliongoza shughuli nzima ya utoaji wa msaada huo alisema kuwa, Tunafahamu umuhimu wa mazingira bora ya afya kwa ustawi wa jamii. Kupitia msaada huu, tunataka kuboresha hali ya wagonjwa hospitalini na kuwawezesha kupata huduma katika mazingira safi na yenye heshima. Huu ni mwendelezo wa kujitoa kwa Meridianbet katika kusaidia jamii na kuboresha sekta muhimu kama afya.”

Huku kwa upande wa Hospitali ya Kijitonyama walishukuru sana kutembelewa na Meridianbet na wamesema kuwa mashuka hayo yatakuwa msaada mkubwa kwa hospitali yao, hasa kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za muda mrefu, hivyo wanawashukuru Meridianbet kwa kuona umuhimu wa kusaidia sekta ya afya na wanawaomba waendelee na moyo huo wa uzalendo.

Msaada huu wa mashuka ni sehemu ya mpango mkubwa wa kijamii wa Meridianbet, unaolenga kuleta mabadiliko chanya katika sekta mbalimbali, zikiwemo afya, elimu, na michezo. Meridianbet imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii na kuboresha maisha ya Watanzania kupitia shughuli mbalimbali za kijamii.

Kama bado hujajisajili na Meridianbet muda ndio huu sasa, ingia na usuke jamvi lako la leo kwani pesa ni nje nje Jumamosi ya leo, Liverpool, PSG, Real Madrid, Bayern wote wapo uwanjani kukupa pesa. Jisajili hapa.

Meridianbet ni kampuni inayoongoza kwa huduma za michezo ya kubashiri nchini Tanzania, ikijulikana kwa uwekezaji wake mkubwa katika maendeleo ya jamii kupitia michango mbalimbali ya kijamii. Pia Meridianbet inatoa michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Poker, Roulette, Sloti na mengine kibao ambayo unaweza kucheza na kupiga pesa.