The House of Favourite Newspapers

Hospitali ya Tumbi Yanufaika na Msaada wa Vodacom Foundation

0

001.TUMBIMadaktari na Wafanyakazi wa Shirika la Elimu Kibaha, Mkoa wa Pwani wakiwa kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya kuwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya wakati wake”watoto njiti” . Vifaa hivyo vilivyotolewa na Vodacom Foundation kupitia taasisi inayojishughulisha kusaidia watoto hao ya Doris Mollel, thamani ya vifaa hivyo ni zaidi ya shilingi Milioni 6/- 
002.TUMBIKaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha,Robert Shilingi (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya watoto katika Hospitali ya Tumbi Dkt.Andrew Lwali (kushoto) wakipokea msaada wa baadhi ya vifaa vya kuwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya wakati(Njiti) kutoka kwa Maneja wa Vodacom Foundation, Sandra Oswald (kulia) wakati wa hafla fupi ya kukabidhiana vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 6/- katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani vilitolewa msaada na mfuko huo kupitia taasisi ya Doris Mollel.Anayeshuhudia watatu toka kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi inayojishughulisha na watoto hao,Doris Mollel.
004.TUMBIKaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha,Robert Shilingi (kushoto)akimshuhudia Muuguzi wa watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Pwani Tumbi,Linda Makundi akionyesha mfano kwa Maneja wa Vodacom Foundation,Sandra Oswald,Njisi mashine ya Oxgen Concentrator inavyofanya kazi ya kuwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya wakati(Njiti) wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 6/- vilivyotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya kusaidia watoto hao.Katika picha kulia ni Mkurugenzi wa taasisi inayojishughulisha na watoto hao,Doris Mollel.
006.TUMBIMeneja wa Vodacom Foundation, Sandra Oswald akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati (Njiti) Emmanuel Evodius katika hospitali ya Mkoa wa Pwani Tumbi alipofika hospitalini hapo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 6/- kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao vilivyotolewa na Vodacom Foundation,wengine katika picha kushoto ni Mama wa mtoto huyo,Emireta Evodius na Mkurugenzi wa Taasisi ya inayojishughulisha na watoto hao,Doris Mollel.

Leave A Reply