The House of Favourite Newspapers

Hospitali za Rufaa, Mikoa Sasa Mikononi Mwa Ummy

Waziri Ummy Mwalimu alipokuwa Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam leo.

 

HOSPITALI 28 za rufaa na mikoa  nchini zenye watumishi 8,671 na vitanda 7,474  zimeanza kusimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto tangu jana Julai 1, 2018.

Hayo yamesemwa leo na waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu,  alipoifanya ziara katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kukagua miundombinu na huduma za afya.

Amesema malengo makuu ya wizara katika kusimamia hospitali hizo ni kuhakikisha uwepo wa madaktari bingwa na kuboresha miundombinu ya huduma za dharura, afya ya mama na mtoto na huduma za wagonjwa mahututi.

Maamuzi hayo yanakuja miezi kadhaa tangu agizo la Rais John Magufuli kuitaka wizara hiyo kuzisimamia hospitali hizo badala ya TAMISEMI iliyokuwa ikizisimamia hapo awali.

Na Edwin Lindege | Global Publishers.

Comments are closed.