Hot 97 Wakanusha Taarifa Za Kutopiga Muziki Wa Tekashi 69
MTANGAZAJI Ebro Darden wa Hot 97 amekanusha taarifa zilizotolewa na mtandao wa TMZ kuhusu kituo chao cha radio Hot 97 kupiga marufuku nyimbo za rapa Tekashi 69.
Siku ya jana Jumatatu mtandao wa TMZ uliripoti taarifa hiyo na kusema imetoka kwa wamiliki wa redio hiyo marufuku kwa kupiga muziki wa Hip Hop.
Baada ya taarifa hizo kusambaa mtandaoni, mtangazaji Ebro Darden kupitia ukurasa wake wa twitter amekanusha taarifa izo na kusema; “Watu wote wa ngazi za juu hapa Hot 97 wamekanusha kuzungumza na TMZ.”
Comments are closed.