Hoteli Waliyofikia Simba ni Jiwe Haswa

TAYARI mabingwa wa Tanzania, timu ya Simba wameshawasili nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs.

 

Simba imefikia hoteli ya kisasa ya Johannesburg Marriott Hotel Melrose Arch, ambayo chumba cha bei ya chini ni shilingi laki 4, jambo linaloonyesha wazi sasa kuwa kwa bei hiyo ni dhahiri Clatous Chama na Luis Miquissone kwa pamoja ndani ya siku moja tu watatumia zaidi ya shilingi laki 8 kulala wakati ndani ya siku nne watakazokuwepo Afrika Kusini kwa pamoja watumia zaidi ya milioni tatu.

Akizungumza na Championi Jumatano, mratibu wa timu hiyo, Abbas Ally amesema, tayari maandalizi ya hoteli yameshakamilika na kwamba kabla ya timu kuwasili waliandaa hoteli mbili ambazo ni Radisson Blu Hotel Sandton iliyopo Johannesburg na Marriott Hotel Melrose Arch, hii imelazimika kufanya hivyo kwa kutazamia kama lolote likitokea basi wangeweza kuhama kutoka hoteli moja hadi nyingine.

 

“Tayari tumeshaweka mipango yetu sawa na kwamba baada ya kufika tuliandaa hoteli zaidi ya tatu lakini kati yake naweza kukutajia mbili ambazo ni Radisson Blu Hotel Sandton na Marriott Hotel Melrose Arch, hizi ndizo ninauhakika kati ya moja wapo timu itafikia, kuhusu maandalizi mengine kwa sasa siwezi kusema maana yako juu yangu,” alisema Abbas.

Stori: Musa Mateja, Dar es Salaam


Toa comment