Hoyce Temu ajumuika na waathirika wa ukoma Dar
Hoyce Temu akiongozana na kamati nzima ya Miss Tanzania kuelekea kwenye ukumbi wa Nungwi ambapo kuna kambi ya wagonjwa wa ukoma.…Akizungumza na baadhi ya wazee ambao ni kati ya waathirika wa ukoma.…Akiwa na mzee mmoja anayeishi kituoni hapo.
…Akichanganya dawa na Tausi Mwenda, mke wa aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda, kwa ajili ya kuulia wadudu. …Akipulizia dawa kwenye vyumba vya waathirika hao.Tausi Mwenda (mwenye shati nyeupe) akiwa ameshika maji kwa ajili ya waathirika hao.Hoyce akila na watoto wa kituo hicho.…Akisaidiana katika shughuli mbalimbali na Tausi Mwenda.Watoto wa kituoni hapo wakiwa tayari kwa chakula.
MISS Tanzania 1999, Hoyce Temu, jana alijumuika na waathirika wa ugonjwa wa ukoma kwenye kambi yao iliyopo Nungwi, Kigamboni, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo alikunywa na kula nao kwa ajili ya kuadhimisha mwaka mpya wa 2016.
Mrembo huyo ambaye aliongozana na kamati nzima ya Miss Tanzania ambapo walifanya usafi katika nyumba za waathirika hao kwa kupuliza dawa za wadudu kama mende, kunguni (Viuatilifu) na kadhalika na baadaye kukaa nao kwa siku nzima.
NA IMELDA MTEMA/GPL