HOYCE TEMU APATA PIGO KUBWA

Hoyce Temu

MISS Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu amepata pigo kubwa baada ya kufiwa na mtoto wake wa kike aitwaye Rania akiwa na umri wa miezi miwili aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Hoyce alisema kuwa amepata pigo kubwa mno ukizingatia mtoto wake huyo aliugua kwa tatizo hilo la moyo tangu alipozaliwa. “Nina huzuni kubwa sana moyoni kumpoteza binti yangu. Nilijaribu kumuokoa maisha yake ikashindikana kwani tulimsafirisha mpaka Afrika Kusini, lakini Mungu amempenda zaidi,” alisema Hoyce.

Mtoto Rania alizikwa wikiendi iliyopita kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi –Amina.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Toa comment