HUDDAH AKATAA KULINGANISHWA NA VERA SIDIKA

‘Huddah Monroe’

MJASIRIAMALI Alhuddah Njoroge, ‘Huddah Monroe’ amekataa kushiriki Tuzo za Black Entertainment Film Fashion Television and Arts (BEFFTA) ambapo yupo kipengele cha International Film and Fashion ambacho hasimu wake Vera Sidika pia amechaguliwa kushiriki na kusema kuwa hawezi kulinganishwa naye hata kidogo. Kwa kutumia mtandao wake wa kijamii, Huddah amekataa kabisa kushiriki katika tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika mwezi huu nchini Uingereza.

“Mmenichagua katika tuzo ambazo wala sizifuatilii kabisa nipo bize na mambo yangu na ninafanya mambo yanayonihusu na sipo kwa ajili ya kulinganishwa na hao mlioniweka nao, kwa Afrika sina wakulinganishwa naye yaani sijaona labda USA (Marekani), nipo bize na brand yangu ya HUDDAH na kuangalia vipi naikuza sitaki ushindani na mtu,” aliandika Huddah.

Loading...

Toa comment