The House of Favourite Newspapers

Huddah: Nimetembea na Kila Aina ya Wanaume

0

MSANII wa muziki, mwanamitindo na mfanyabiashara kutoka Kenya, Huddah Monroe, amefunguka na kusema kwamba ameshatembea na kila aina ya wanaume, hivyo kwa sasa yupo tayari kuzaa na kulea watoto wake.

 

“Najua mwanaume wangu unaiangalia hii, mwanamke bora wa kumuoa ni mimi Madam Alhuda. Acha nijipigie talumbeta, nimeona kila kitu niko tayari kuwa mama wa watoto wa 5” amesema Huddah socialite maarufu wa Kenya na kuongeza.

 

“Hawa wanawake wanaotoka na wavulana nalaumu sana ujana wao, hawakufurahia maisha. Nimetoka kimapenzi na Wachina, Wahindi, Wanaigeria, Wakenya. Kipindi nina miaka 21 nilijaribu kila kitu.

 

“Nilikuwa najiuza na kutembea kufuata wanaume sehemu mbalimbali, sasa hakuna cha kunistaajabisha. Namtanzama mwanaume jinsi alivyo sio alichonacho kwenye kaptula yake, nimeona ya kila aina,” amesema Huddah.

 

Leave A Reply