The House of Favourite Newspapers

Huduma ya Kibenki kwa Wanafamilia ni Moja ya Nguzo za Kihuduma za Benki ya Stanbic Tanzania

0
Meneja Mkufunzi wa Benki ya Stanbic Tanzania upande wa wateja Maalum, Irene Bizere, akitoa mafunzo ya kuweka akiba kwa baadhi ya watoto wa wateja maalum wa benki hiyo, Mafunzo hayo yalifanyika jijini Dar ers Salaam.

Dar es Salaam, Tanzania – Agosti 2024:Idara ya wateja maalumu ya Benki ya Stanbic Tanzania  inajivunia kuwa na huduma ya stadi za awali ya elimu ya  kifedha kwa wanafamilia hasa watoto na vijana. Tukio hilo lilifanyika jumamosi iliyopita katika Tawi lao la Peninsula huko Masaki.

Huduma hiyo imeanzishwa ili kuwapatia  watoto  ujuzi  wa kifedha, ikiwemo njia mbalimbali za kutafutafedha, matumizi sahihi ya fedha, utunzaji na akiba binafsi. Kwa kuwapatia watoto elimu ya kifedha, Benki ya Stanbic Tanzania inatarajia kuwajengea  nidhamu na uelewa wa kifedha  unaohitajika katika utunzaji wa fedha kwa ujumla.

Mshauri Mwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Richi Ndisi akitoa mafunzo ya matumizi ya fedha kwa baadhi ya watoto wa wateja Maalum wa benki hiyo, Mafunzo hayo yalifanyika jijini Dar es salaam.

“Tunaamini kwamba ujuzi wa kifedha ni ujuzi muhimu wa maisha ambao unapaswa kukuzwa tangu umri mdogo,” alisema Irene Bizere,Meneja wa Wateja Maalumuwa Benki ya Stanbic Tanzania.“Kupitia mpango huu, tulilenga kuwezesha kizazi kijacho kwa maarifa na zana wanazohitaji kwa kufanya maamuzi sahihi ya kifedha.”

Tukio hili lilikuwa na aina mbalimbali za mafunzo shirikishi yaliyoimarisha dhana za kifedha ambazo watoto walikuwa wameelimishwa. Mojawapo ya stadi walizofundishwa vijana hao ilikuwa kupanga bajeti.Mafunzo yaliendeshwa kwa njia ya vitendo kupitia uigizaji ya namna bora ya utunzaji wa fedha.

Mafunzo kama haya yana faidi nyingi ambazo watoto watakuwa nazo hadi umri wa mtu mzima. Zaidi ya hayo, watoto walio na ujuzi wa kifedha wana uwezekano mkubwa wa kuepuka madeni yasiyo ya lazima, kujiokoa kwenye matukio muhimu ya maisha, na hivyo  kuchangia vyema katika uchumi wa nchi yetu na kuwapatia suluhisho mbalimbali.

“Mpango huu unasisitiza dhamira yetu na sio kuwapatia suluhisho za kifedha wateja lakini pia kuwapa wapendwa wao na wanafamilia wao huduma kama hii,” aliongeza Irene.”

Leave A Reply