Huduma ya Kufanya Mapenzi Kwenye Ndege Tsh Mil 2

Kampuni ya ndege binafsi ya nchini Marekani ya Love Cloud imeanza kutoa huduma kwa wapenzi wanaohitaji kushiriki tendo la ndoa kwenye anga la Las Vegas wakiwa kwenye ndege za kampuni hiyo.

 

Kwa mujibu wa Kampuni ya Love Cloud, huduma hiyo itachukua dakika 45 ambapo wapenzi wanaoshiriki tendo la ndoa watatakiwa kulipa dola 995 za Kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 2 ili kufurahia penzi lao wakiwa angani.

Hata hivyo kwa wapenzi watakaotumia saa moja na zaidi kufanya tendo la ndoa katika ndege hiyo basi watalazimika kulipia dola 1,495 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 3.

 

Sheria nchini Marekani haziwaruhusu abiria kufanya tendo la ndoa kwenye ndege, lakini kampuni hiyo ya ndege binafsi imepata kibali maalumu cha kutoa huduma hiyo katika anga la Las Vegas nchini humo pekee!


Toa comment