Huduma za TIC Mpaka Kasulu,Kigoma

Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Kanda za Nyanda za Juu Kusini Bw. Venancy Mashiba, amesema Kituo hicho kimefanya tafiti mbali mbali ya zao la michikichi na kuibua fursa zake na kwamba kwa sasa wanashawishi wawekezaji kuja Kigoma kwa lengo la kuanzisha miradi ya zao la mchikichi kuanzia hatua ya kilimo mpaka uchakataji nchini.

Hatua hiyo itapandisha thamani ya zao hilo na kuwezesha wakulima wa zao hilo kuongeza kipato na kuiwezesha Serikali kuongeza ajira pia kupunguza gharama za kuagiza mafuta nje ya nchi.

Hayo yameelezwa katika maeonyesho ya Tatu ya SIDO Kitaifa yanayoendelea Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma mpaka tarehe 30 Septemba, 2021.


Toa comment