The House of Favourite Newspapers

Hujui? Wee mwenyewe ndo’ unamchepua mwenzio!

0

julianadidone3Leo shoga nina hasira na akina mama wanaodorora kwenye mahanjamu, ambao hawajui muda wa mume kupata chakula cha usiku au hawawapi nafasi waume zao pale wanapowahitaji.

Kutokana na hasira hizi hata salamu naona ngumu kuwapa kwani pointi zangu zitayeyuka, hivi mashosti hamjui mwanaume akishakuwa na stimu ya kula chakula hutakiwi kumkatisha?

Ndiyo maana wengi wenu mnalalamika kutoridhika, mara ooh mume wangu hana hamu siku zote.

Atakuwaje na hamu wakati akiwa nayo unamdengulia? Naamua kuwapa live wanawake wenzangu kwa sababu nimepata mada hii kutoka kwa wasomaji tofauti huku mmoja akimlalamikia mkewe kujishughulisha na kazi mpaka usiku wa manane, hasa yeye akishajua kuwa mume anamhitaji.

Akiitwa utasikia nakuja, nakuja, nakuja zinakuwa nyingi sana mpaka mume anasinzia na kujikuta akikasirika.

Mwanamke mwenzangu kwanza huoni ufahari mume kukuhitaji faragha? Wapo wanaolia kuwa waume zao hawana muda na wao na wengine wanalia na kusema kila akimuomba mume anamwambia amechoka.

Niwaambie tu wanawake wenzangu, hakikisha unafanya kazi zako zote muda ambao mume wako hajafika nyumbani kwani muda wowote anaweza kukuhitaji.
Kwanza ukumbuke kuwa ni dhambi kumkatalia mume wako unyumba kwani hiyo ndiyo maana halisi ya ndoa.

Hivi shosti mpaka saa saba usiku huendi chumbani kwa mumeo anakusubiri unakuwa unafanya nini hasa?

Akienda kuchepuka utamlaumu kweli? Uwe umekasirika uwe huna hamu ni lazima uende chumbani kwa mumeo, utaipataje hamu ukiwa mbali naye.
Nikukumbushe tu shosti chanzo cha matatizo siku zote huanzia hapo kwani mume anaweza kuhisi nawe una kamchepuko kanakokusababisha ukawa huna hamu ya kuwa naye faragha.

Mwanamke unayefanya hivyo jiangalie upya, usije kuachwa na kukesha kwa waganga ambao hawawezi kukusaidia lolote zaidi ya kukumalizia hela.
Utajikuta unajutia yote uliyowahi kumfanyia mumeo ambayo kwa sasa unayaona ni madogo.
Kwa leo naishia hapa, nashukuru mlionitumia ujumbe. Hapa nitaandika yanayoandikika mengine tutamalizana kwa simu tu!

Wapendwa wasomaji namba hii ni kwa ajili ya mwenye tatizo linaloweza kuandikwa tu na tutaandika hapa kwa faida ya wengine, nawasihi msitumie namba hii vibaya kwani wapo wanaodhani imewekwa kwa mzaha.

Leave A Reply