The House of Favourite Newspapers

Huku Drama za Diamond na Wema Zikinoga, Kule Zari Bata Batani – Picha 7

WAKATI Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz akiendeleza drama ya mapenzi na aliyekuwa girl friend wake, Wema Sepetu kupitia mitandao ya kijamii, mzazi mwenzake na mwanamuziki huyo, Zari The Bosy Lady ameendelea kura raha katika Hoteli ya Sun City nchini Afrika Kusini anakoishi.

Zari kupitia ukurasa wake wa Instagram ametupia picha saba akila bata katika hoteli hiyo kuonyesha kuwa haumizwi na kile anachokifanya x wake huyo mitandaoni kwa kujiweka karibu na Wema, kupost picha na maneno yanayoonyesha kuwa wamerudisha uhusiano wao.

Zari baada ya kuweka picha hizo hakuandika maneno mengi bali ameweka caption hii; Sun City typa weekend.

Kuanzia jana Ijumaa kumekuwa na drama mitandaoni zikionyesha Wema na Diamond kama tayari wamesharudiana baada ya Wema kutupia picha na kipande cha video mpya ya Diamond, African Beauty na kumfagilia boy friend wake huyo wa kitambo.

Wema aliandika “I’m inlove with you there’s nothing dat I wouldn’t do, catch a grenade for you, as long as you want me to…” jambo lililomuibua Diamond na kuanika bila kificho mahaba yake kwa Wema.

Zari na Diamond waliachana mwezi uliopita kwa kile kilichodaiwa na mwanamama huyo kuwa sababu ni Diamond kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

 

Na Edwin Lindege.

Vilio Vyatawala, Mazishi ya Mmiliki wa Super Sami, Aliyeokotwa Mtoni

Comments are closed.