The House of Favourite Newspapers

Huku Makambo, Kule Kazadi Kitawaka Ligi Kuu

0

KWA namna kikosi cha Yanga kinavyosuka kuelekea msimu ujao wa 2021/22, ni wazi wapinzani hawatoki salama kila wakiingiza mguu uwanjani kuwania pointi tatu.


Hiyo ni baada ya
mshambuliaji wa zamani wa AS Vita, Francis Kazadi kukubali kutua Yanga iwapo tu klabu hiyo itakamilisha taratibu zote za usajili wake.

Kazadi kwa sasa anakipiga
Wydad Casablanca ya Morocco ambapo anacheza sambamba na Mtanzania, Simon Msuva aliyewahi kuichezea Yanga.

 

Wiki iliyopita, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said, alikuwa nchini Morocco alipoenda kufanya ziara, huku akifanikiwa kuonana na Msuva.

Kuhusu kuhitajika ndani ya Yanga na kuwa katika mazungumo nao, Kazadi aliliambia Spoti Xtra: “Nipo tayari kujiunga na timu yoyote ambayo italeta ofa nzuri kwangu.“Yanga kuna mazungumzo ya awali ambayo hayajakamilika kwa sasa na kama watayakamilisha sina shida nao, mpira ndio kazi yangu, nitakubali kujiunga nao.

 

Yanga licha ya kuwa katika mazungumzo na mchezaji huyo, pia inahusishwa na usajili wa washambuliaji wengine wawili, Heriter Mkambo ambaye tayari ni mchezaji huru akimalizana na Horoya AC ya Guinea.

 

Mwingine anayetajwa Yanga ni Fiston Mayele ambaye ameweka wazi kuwa hivi karibuni atatua nchini kwa ajili ya kukamilisha dili lake hilo.Endapo Yanga watafanikiwa kukamilisha usajili wa washambuliaji hao wote, ni wazi msimu safu yao ya ushambuliaji itakuwa na makali sana kulinganisha na msimu huu.

 

Safu hiyo itakuwa na watu wenye njaa ya mabao ambao ni Fiston Mayele, Heritier Makambo, Francis Kazadi na Yacouba Songne.

 

Msimu uliopita, Mayele alishika nafasi ya pili kwa ufungaji ndani ya Ligi Kuu ya DR Congo baada ya kufunga mabao 13, huku Kazadi akifunga mabao 9 katika micheo 14 aliyoichezea Wydad Casablanca, huku msimu wa 2018/19 akiwa AS Vita, aliifungia klabu yake mabao 18 katika michezo 30.

 

Makambo anakumbukwa ndani ya Yanga alipocheza msimu mmoja wa 2018/19 ambapo alifunga mabao 21 na kutoa asisti 4 katika michezo 39 ya michuano yote.

STORI: MARCO MZUMBE, DAR ES SALAAM

Leave A Reply