The House of Favourite Newspapers

Huku Upepo wa Kisulisuli… Wema Aitosa Mahari ya Rubani

WAKATI wanawake kibao wakikimbilia kuwapata waume wanaoletwa na upepo wa kisulisuli katika Kanisa la Mlima wa Moto la Mchungaji Dk Getrude Rwakatare ‘Mama Rwakatare’, mrembo kutoka Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ameitosa mahari ambayo ilikuwa itolewe na rubani wa ndege, Hamdan Zakwani ‘Danzak’.

 

ISHU ILIPOANZIA…

Inakumbukwa mapema mwaka huu, rubani huyo ambaye pia hufanya muziki wa Bongo Fleva alijitosa mzimamzima kutaka kumuoa Wema kwa kueleza kuwa ndiye chaguo la moyo wake kwamba yupo tayari kwa lolote endapo Wema na familia yake wataridhia.

 

ALIKUWA ‘SERIOUS’

Danzak alionesha kweli amedhamiria kwani alipofika nchini, aliwatuma marafiki na ndugu zake wa karibu waende kupeleka posa nyumbani kwa mama Wema na mipango ikienda vizuri basi amuoe.

 

TUPATE HABARI KAMILI

Mapema wiki hii, Ijumaa lilikutana uso kwa uso na Wema alipokuwa kwenye hafla ya uzinduzi wa duka jipya la viatu la shosti wake Aunt Ezekiel maeneo ya Bamaga- Mwenge jijini Dar ambapo alifungukia mambo mbalimbali likiwemo hilo la kukataa kuolewa na Danzak.

 

HUYU HAPA MADAM…

Alipoulizwa kuhusu Danzak ambaye Januari mwaka huu, aliupamba ukurasa wa mbele wa Gazeti la Ijumaa Wikienda na kichwa cha habari kilichosomeka; RUBAN AJITOSA KUMUOA WEMA, mrembo huyo alisema alimuona jamaa huyo lakini yeye hakuwa tayari kuolewa naye.

 

“Ni kweli nilimuona, ni kijana mzuri ambaye kweli inaonesha alikuwa na nia njema na mimi lakini kwa kweli binafsi sikuwa tayari kuolewa naye,” alisema Wema na kuongeza.

“Kwa kweli hajakidhi vigezo ambavyo mimi nahitaji kuviona kutoka kwa mwanaume ambaye anataka awe mume wangu.”

 

MUZIKI NDIO ULIMKATA STIMU

Kwenye mahojiano hayo maalum na Ijumaa, Wema alisema awali alikuwa kwenye mkao wa kusubiri mahari baada ya kuona jamaa huyo amejitosa kwa kuwa kweli hakuwa na mtu wakati huo lakini alipokuja kugundua kwamba anajishughulisha na muziki, aliishiwa pozi sababu hafikirii kuolewa na msanii.

“Nilivunjika sana moyo kwa kweli baada ya kuona tena ni msanii yaani sijui nisemeje lakini kwa kweli nilianza kuona kwamba hawezi kuwa siriazi, angekuwa na hiyo kazi ya urubani pekee ningejaribu kumfikiria mara mbili,” alisema Wema.

 

ANAYAKUMBUKA YA MONDI?

Alipoulizwa kama alimtolea mbavuni jamaa huyo kwa kumbukumbu za aliyewahi kuwa mpenzi wake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Wema alisema hapana bali amekataa kutokana na mtazamo wake tu wa sasa na wala haihusiani na kumbukumbu hiyo.

 

MWANAUME WAKE NI NANI?

Ijumaa lilizidi kumchimba mrembo huyo ambaye kwa sasa amejikondesha na kupoteza ule muonekano wake wa u-kibonge ili kuweza kumjua mwanaume wake wa sasa baada ya kuwa ‘singo’ kwa muda mrefu.

“Hahaha siwezi kukuambia ni nani lakini kiukweli mwanaume ninaye kwa sasa, acha tu iwe private kwa sasa mpaka hapo baadaye nitakapoona inafaa kumuanika nitafanya hivyo,” alisema Madam.

 

WALIWAHI KUNASWA HOTELINI

Licha ya Wema kumchomolea rubani huyo, Wema aliwahi kuonekana na jamaa huyo wakiingia hotelini Machi, mwaka huu na picha yake ikapamba ukurasa wa mbele wa gazeti ndugu na hili la Amani lililokuwa na kichwa cha habari kilichosomeka; WEMA, RUBANI WANASWA HOTELINI.

Kwenye habari hiyo, wawili hao walionekana wakiingia pamoja na kupeana kampani hotelini lakini haikufahamika dhumuni lao hotelini hapo.

 

DANZAK NI NANI?

Danzak ni Mtanzania, ambaye kabla ya kwenda masomoni nje ya nchi amewahi kufanya kazi za muziki katika Kundi la TNG Squard lililokuwa likiundwa na wasanii Agustino John ‘Latino Man’ na Malicki Bandawe.

 

Baadaye jamaa huyo alikwenda kusomea urubani na kufanikiwa kuhitimu kisha kuajiriwa kwenye shirika moja kubwa la ndege Uarabuni ambapo analitumikia hadi sasa.

 

Mbali na kurusha ndege, rubani huyo shughuli za kimuziki bado ziko kwenye damu na alipofika Bongo mapema mwaka huu, kwa siku chache aliweza kutunga na kurekodi nyimbo mbili ambazo ni Fall In na Kichaa kisha akarudi Uarabuni kuendelea na kazi yake ya urubani.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.