The House of Favourite Newspapers

Hukumu Kesi ya Sabaya Yaahirishwa

0

 

HUKUMU ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili iliyokuwa itolewe leo , na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirishwa hadi Oktoba 15, 2021.

 

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa Oktoba mosi, 2021 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Amalia Mushi.

 

Sabaya na wenzake, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, wanakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha. Inadaiwa katika shtaka la kwanza kuwa Februari 9, 2021 katika Mtaa wa Bondeni, Arusha, washtakiwa hao waliiba Sh2.769 milioni, mali ya mfanyabiashara Mohamed Saad.

 

 

Leave A Reply