The House of Favourite Newspapers

Humphrey Polepole Azindua Ukarabati Mkubwa Uwanja wa CCm Kirumba- Mwanza

0

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amezindua rasmi ukarabati wa Uwanja wa Soka wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo amesema kwamba chama chake kitahakikisha uwanja huop unaendelea kuwa na hadhi ya juu inayokubalika na FIFA.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Mwanza, alisema karibu asilimia 70 ya viwanja vyote vya soka nchini, vinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), jambo linalodhihirisha kwamba CCM siyo chama cha siasa tu bali chama kinachoijali jamii kwa kila kitu.

 

Polepole alisema tofauti na viwanja vingine viokubwa ambavyo huwekwa nyasi bandia, wao wameamua kupanda nyasi halisi ambazo zitakuwa zikitunzwa kwa uangalizi wa hali ya juu kuhakikisha uwanya unakuwa na ‘pitch’ yenya hadhi ya kimataifa.

Leave A Reply