HURUMA ILIYOJE! DIAMOND Ampa Bajaj Mama Mlemavu – Video
MSANII Nyota wa Bongofleva Naseeb Abdul “Diamond Platnumz” ameompa zawadi ya bajaj mpya mama mwenye ulemavu wa miguu, Bi. Evodia Nchimbi, mkazi wa Mburahati jijini Dar es Salaam wakati wa birthday ya msanii huyo nyumbani kwao Tandale leo Ijumaa, Oktoba 5, 2018.
Bi. Evodia ambaye ni dereva bajaj alikuwa akiendesha bajaj ya mtu mwingine na kujipatia kipato na sasa Bajaj hyo mpya itakuwa ya kwake na itamsaidia kufanya biashara yake ya kubeba abiria ikiwa ni sehemu ya kujiingizia kipato aweze kujikwamua katika na kuendelea kuitunza familia yake.
Baada ya kupewa zawadi hiyo, Bi. Evodia alimshukuru huku akitoa machozi na kutoamini kwa kile kilichotokea, huku akisema kwamba agalau sasa ataweza kuwa na ahuweni ya maisha.
Comments are closed.