Husna: Niacheni Nile Makombo Yangu Mwenyewe!
Stori: Imelda Mtema | RISASI JUMAMOSI | Dar es Salaam
MREMBO aliyewahi kunyakuwa Taji la Miss Kinondoni 2011, Husna Maulid amewacharukia watu wanaomsema kwamba anakula makombo ya wasanii wenzake kwa mchumba wake Mwami Rajabu, ambaye ni raia wa Kongo kwa kuwataka wamuache kama alivyo.
Husna alisema amekuwa akipigwa sana vijembe kwenye uhusiano wake huo lakini hakuna hata moja analolisikiliza na kuliweka kichwani kwani ameziba masikio hasikii kitu chochote kwa kuwa mpenzi wake huyo ndiyo chaguo lake.
“Kama ni makombo nakula ni mimi, waniache. Kuna mambo mengi sana nimesikia kuhusiana na mahusiano yetu na Mwami, lakini mimi ni mwanamke shupavu naangalia zaidi moyo wangu na si kitu kingine chochote,” alisema Husna.
Comments are closed.