HUU NDIYO UKWELI UWOYA KUPORA MUME WA MTU

Irene Uwoya

DAR ES SALAAM: Ile skendo kabambe iliyozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na staa wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya kupora mume wa mtu, mwenyewe ameanika ukweli wa ishu hiyo.  

 

Mapema wiki hii zilivuja picha kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha Uwoya ‘akijibebisha’ kwa mwanaume ambaye ilisemekana ni mume wa mtu kisha kuunganishwa na ile ahadi yake ya wiki mbili zilizopita ambapo aliahidi kupora mume wa mtu kwa madai kwamba naye aliporwa wa kwake.

 

Katika mahojiano maalum na Ijumaa, Uwoya ‘alibanwa mbavu’ ili kuweka wazi mbivu na mbichi za skendo hiyo ambapo alisema anawashangaa watu siku zote wanaweza kukiona kitu, lakini hawatumii hata muda kidogo kukifanyia uchunguzi badala yake wanakurupuka na kuweka vitu visivyokuwa na uhakika mitandaoni.

 

“Ndiyo maana siku zote mimi nawaambia watu waache unafiki maana wako macho kuona Irene (Uwoya) anaharibu, lakini wanashindwa kufuatilia ukweli wa jambo hilo hata kidogo tu,” alisema Uwoya. Akiendelea kuzungumza na Ijumaa, Uwoya alisema huyo anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu ni mjomba wake kabisa na hata kwenye hiyo harusi alikuwa na mke wake, sasa hajui kwa nini watu waseme alikuwa na mume.

 

“Yule ni mjomba wangu kabisa jamani, inakuwaje anakuwa mwanaume wangu? Huko si ni kuvinjiana heshima? Tena kubwa na isitoshe mjomba wangu huyo alikuwa na mke wake, lakini kwa sababu watu wanapenda kufuatilia mambo, wakaibuka na hivyo,” alisema Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Krish.

 

Uwoya alisema anajua wazi kuwa alivyoweka ile picha kuna watu watatafuta vya zaidi na ndiyo kama hivyo walivyojiongeza wenyewe na kudai ni mume wa mtu. “Nilijua tu ndiyo maana nikamziba sura, kuna wanafiki watajitokeza na kuyaleta yao, lakini kwa hapo wamefeli na tena kama ni mtihani wamepata F au ziro kabisa,” alimalizia Uwoya ambaye hivi karibuni aliachana na Dogo Janja.

Stori: Imelda Mtema, Ijumaa

Toa comment