Huyo Kocha wa Manula Kazi Anayo Simba

KUONESHA kwamba hataki masihara hata kidogo juu ya makipa wake, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck ametangaza atamfanyia usaili wa ana kwa ana kocha mpya wa makipa wa timu hiyo.

 

 

Kocha huyo ameongeza kwamba, atafanya usaili huo wa kumchagua kocha ambaye atawafundisha makipa wake wanaongozwa na Aishi Manula kwa sababu anataka kocha bora ambaye atafanya kazi naye vizuri ikiwa ni baada ya kupokea CV za makocha wengi wakiomba kazi hiyo.

 

 

Simba kwa sasa wanasaka kocha wa makipa baada ya hivi karibuni kusitisha mkataba wa Muharami Mohammed ambaye ndiye aliyekuwa kwenye nafasi hiyo.

 

 

Sven amesema licha ya kupokea CV za makocha wengi, lakini kwake hatajali sana kuhusiana na hizo ambapo atafanya usaili huo wa ana kwa ana kwa ajili ya kuangalia ubora wa anayeomba japokuwa kwake haitakuwa kazi ndogo.

 

 

“Tumepokea CV (wasifu) wa watu wengi, kwa sababu watu wapo huru kutuma lakini CV haisemi kila kitu, nataka kumuona jinsi anavyofundisha na mazoezi yake.

 

 

“Tunataka kocha bora na ambaye atakuja kurudisha ushindani kwa makipa, nitaongea nao sura kwa sura japokuwa haitakuwa kazi ndogo,” alimaliza kocha huyo raia wa Ubelgiji.

SAID ALLY, Dar es Salaam

 Tecno


Toa comment